logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kiungo wa Arsenal Mohammed Elneny aanzisha klabu yake baada ya kusahaulika na Arteta

Maono ya akademia ni ya moja kwa moja: kuziba pengo kati ya soka ya ngazi ya chini na ya kulipwa,

image
na Davis Ojiambo

Michezo17 October 2023 - 03:57

Muhtasari


  • • Elneny FC itatoa njia iliyopangwa kwa vijana wenye vipaji wenye umri wa miaka 5-16 na 16-25 kubadili kutoka kwa soka isiyo ya ligi hadi safu ya kulipwa.
Mohammed Elneny.

Kiungo wa kati wa Arsenal Mohamed Elneny amezindua klabu yake ya soka, jarida la London World limesema.

Elneny FC itatoa njia iliyopangwa kwa vijana wenye vipaji wenye umri wa miaka 5-16 na 16-25 kubadili kutoka kwa soka isiyo ya ligi hadi safu ya kulipwa.

Maono ya akademia ni ya moja kwa moja: kuziba pengo kati ya soka ya ngazi ya chini na ya kulipwa, na akademi hiyo ikikuza talanta mapema kama miaka 5 na , ikiendelea kuongoza maendeleo yao wanapofikisha miaka 16.

Mchezaji wa kimataifa wa Misri Elneny, ambaye ana leseni B ya UEFA, anashiriki kikamilifu katika baadhi ya vikao vya kufundisha, akileta uzoefu wake mkubwa kama mchezaji wa Ligi Kuu ili kunufaisha vipaji vya vijana.

Kwa kutoa mwongozo uliopangwa, utaalamu wa kufundisha, na kujitolea bila kuyumbayumba, analenga kuunda mustakabali wa maendeleo ya soka, jarida hilo lilisema.

"Lengo langu ni kufikia ndoto za wachezaji watoto na kuboresha uchezaji wao katika kandanda pamoja na kuwasaidia kufikia kiwango cha juu."


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved