logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Saudi Arabia yatarajiwa kuandaa Kombe la Dunia 2034 baada ya Australia kujiondoa

Saudi Arabia ndio taifa la pekee lililowasilisha ombi

image
na Radio Jambo

Yanayojiri31 October 2023 - 12:27

Muhtasari


•Shirikisho la Kandanda Australia ilithibitisha uamuzi wake saa chache kabla ya tarehe ya mwisho ya Fifa kutangaza ombi hilo Jumanne.

•Morocco, Ureno na Uhispania zitakuwa mwenyeji wa dimba la 2030, na mechi pia zitachezwa nchini Argentina, Paraguay na Uruguay.

Saudi Arabia iko tayari kuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia la 2034 baada ya Australia kuamua kutowasilisha ombi la kutaka kuandaa mashindano hayo.

Shirikisho la Kandanda Australia ilithibitisha uamuzi wake saa chache kabla ya tarehe ya mwisho ya Fifa kutangaza ombi hilo Jumanne.

Saudi Arabia ndio taifa la pekee lililowasilisha ombi

"Tumefikia hitimisho la kutofanya hivyo kwa mashindano ya 2034," ilisoma taarifa kutoka kwa Soka Australia.

Kombe la Dunia la 2026 litafanyika Marekani, Mexico na Canada.

Morocco, Ureno na Uhispania zitakuwa mwenyeji wa dimba la 2030, na mechi pia zitachezwa nchini Argentina, Paraguay na Uruguay.

Saudi Arabia imekuwa mwenyeji wa hafla kadhaa kuu za michezo tangu 2018, zinazohusisha mpira wa miguu, mashindano ya magari ya Formula One , mchezo wa gofu na ndondi.

Mwanamfalme Abdulaziz bin Turki bin Faisal, waziri wa michezo wa Saudi Arabia, alisema ombi la Kombe la Dunia "ni hatua muhimu na ya asili katika safari yetu kama nchi inayopenda soka".

Ufalme wa Ghuba umeshutumiwa kwa kuwekeza katika michezo na kutumia matukio ya hali ya juu ili kuboresha sifa yake ya kimataifa - mchakato unaojulikana kama kuosha ‘uchafu’ kwa kutumia michezo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved