logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Mamangu anafikiri wewe ni mtanashati!" shabiki wa kike amuinulia Bukayo Saka bango

Shabiki huyo alisema ujumne huo ni kutoka kwa mama yake kwa Saka.

image
na Davis Ojiambo

Michezo18 November 2023 - 11:16

Muhtasari


  • • “Saka, mama yangu anadhani wewe ni mtanashati," ujumbe unasoma.
  • • Saka ni sehemu muhimu ya Three Lions ya Gareth Southgate lakini alianza kutokea benchi dhidi ya Malta
Bukayo Saka,

Winga wa Arsenal, kinda Bukayo Saka ni moja ya wachezaji pendwa Zaidi kwa sasa nchini Uingereza sit u na mashabiki wa Kiafrika kutokana na ngozi yake nyeusi bali pia na mashabiki wa UIngereza.

Wengi wanampenda kutokana na ufundi wake uwanjani lakini pia imeibuka kwamba kuna baadhi ya mashabiki wa kike ambao wanasinzia na kuwaza kutoka kimapenzi na mchezaji huyo anayeiwajibikia timu ya taifa ya Uingereza licha ya kuwa na usuli wa Nigeria.

Usiku wa Ijumaa katika mechi ya kimataifa baina ya UIngereza na Malta, shabiki mmoja wa kike alionekana na bango uwanjani akimuonesha hadharani na mubashara Bukayo Saka mapenzi.

Shabiki huyo mrembo aliingia uwanjani katika mechi hiyo ambayo Uingereza walishinda kwa urais mabao 2-0 dhidi ya Malta, akiwa na bango la kuwasilisha ujumbe wa mamake kwa Saka.

Bango hilo lilisoma kwamba mamake shabiki huyo ana kila sababu ya kufikiria kwamba Bukayo Saka ni mchezaji mtanashati Zaidi, si tu uwanjani lakini pia kwa muonekano wa sura yake.

“Saka, mama yangu anadhani wewe ni mtanashati," ujumbe unasoma.

Saka ni sehemu muhimu ya Three Lions ya Gareth Southgate lakini alianza kutokea benchi dhidi ya Malta na kuingia kipindi cha pili kwa nyota wa zamani wa Chelsea, Fikayo Tomori.

Alisaidia mshambuliaji wa Bayern Munich, Harry Kane kufunga bao la pili na kusaidia nchi yake kuona ushindi huo katika kiwango cha chini cha waliofuzu fainali za Euro 2020.

Iliisaidia timu hiyo kuendeleza uongozi wao wa pointi sita kileleni mwa Kundi C dhidi ya Italia na Ukraine, zote zikiwa na pointi 13 kila moja hadi pointi 21 za Uingereza.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved