John Obi Mikel azungumza kuhusu wachezaji wa Kiafrika kutuma pesa kwa familia nyumbani

Obi Mikel anasema wanasoka wa Afrika wanatozwa kodi ya ziada kwani mara nyingi wanasaidia familia na marafiki nyumbani.

Muhtasari

•John Obi Mikel amedai kuwa baadhi ya wachezaji hata "wanatishiwa na familia zao" ikiwa hawatatoa msaada wa kifedha.

•Mikel anasema wachezaji wanapaswa kuwa na nguvu ikiwa wataamua kuacha kusaidia wengine kifedha, kwani kunaweza kuwa na upinzani.

alikuwa nahodha wa Nigeria kwenye Kombe la Dunia la Fifa 2018 nchini Urusi, ambapo Super Eagles waliondolewa katika hatua ya makundi.
John Obi Mikel alikuwa nahodha wa Nigeria kwenye Kombe la Dunia la Fifa 2018 nchini Urusi, ambapo Super Eagles waliondolewa katika hatua ya makundi.
Image: BBC

John Obi Mikel anasema wanasoka wa Afrika wanatozwa kodi ya ziada kwani mara nyingi wanasaidia familia na marafiki nyumbani.

Kiungo huyo wa zamani wa Chelsea na Nigeria amedai kuwa baadhi ya wachezaji hata "wanatishiwa na familia zao" ikiwa hawatatoa msaada wa kifedha.

"Unapotoka Afrika - na hili ni jambo ambalo sidhani tunazungumza sana - unapopata pesa, sio pesa yako," Mikel alisema, akizungumza kwenye kipimndi cha radio cha Rio Ferdinand vibe with FIVE.

"Una jamaa wote hawa familia, binamu, kila mtu .

"Dada zako, wanaenda na kuolewa na kijana fulani ambaye lengo lake ni kuoa tu katika familia ya John Obi Mikel kwa sababu basi [anafikiri] 'maisha yake yatakuwa mazuri '.

“Unaanza kumuangalia huyu jamaa na unamtumia pesa dada yako na pesa inaenda kwake anafanya chochote anachofanya nazo.

"Hili ndilo jambo ambalo hakuna mtu anayejua - pesa yako sio pesa yako.

"Unapata mshahara na kusema 'nitaweka kando hii kwa ajili ya mtu huyu, niweke kando kwa ajili ya mtu huyo, na kuiweka kando kwa ajili ya mama na baba yangu'. Kabla hujajua, unapata kidogo kuliko wao.

"Huo ndio utamaduni. Wanatarajia ufanye hivyo. Kwao, wanakudai.

"Hadithi hii inahitaji kuelezwa. Wachezaji wengi wa Kiafrika wanaokuja sasa wanahitaji kuambiwa hili kwa sababu watapitia hali kama hizo.

"Watahitaji kujua jinsi ya kukabiliana na hili."

Mikel anasema wachezaji wanapaswa kuwa na nguvu ikiwa wataamua kuacha kusaidia wengine kifedha, kwani kunaweza kuwa na upinzani.

"Wakati mwingine unapaswa kusema 'Inatosha, sijali'. Kwangu wakati huo ulikuja takriban miaka mitano iliyopita," kijana huyo mwenye umri wa miaka 36 aliongeza.

“Nilisema ‘No more’, kwa sababu nimekuwa nikifanya hivi tangu nianze kucheza soka.

"Unakuwa mtu mbaya. Wanaacha kujibu simu zako. Wamezoea kukupigia - sio kukujulia hali bali kuuliza 'Unanipa nini?'.

“Lazima uwe na nguvu za kutosha nilikuwa natoa sana kwa familia.

"Unachofanya ni kuendelea kutoa na wako vizuri sana hivi kwamba wanatarajia ufanye hivyo kwa maisha yako yote."

Mikel anasema wachezaji wanaweza hata kudanganywa kihisia.

"Wanakupa vitisho 'Ikiwa hutafanya hivyo [kulipa], tutaenda kwa waandishi wa habari'.

"Unafikiri, 'Nyinyi ni familia. Baada ya yote niliyowafanyia nyie?'.

"Katika Afrika sio kila mtu anajitokeza na kuzungumza kuhusu hili, kwa sababu tunafikiri 'Tutazungumzaje kuhusu hili?'.

"Unatishiwa na damu yako mwenyewe."

Kesi za utekaji nyara huwaacha wachezaji wakiwa 'wanyonge kabisa'

Mikel aligundua babake alikuwa ametekwa nyara kwa mara ya pili kabla ya Nigeria kuvaana na Argentina kwenye Kombe la Dunia 2018, lakini bado alicheza huku Super Eagles wakichapwa 2-1.

Mikel pia amekuwa akitafakari kuhusu athari za baba yake kutekwa nyara mara mbili, ikiangaziwa kwamba babake mchezaji wa fowadi wa Liverpool Luis Diaz hivi majuzi pia naye alipitia hali kama hiyo.

Babake mchezaji huyo wa kimataifa wa Colombia aliachiliwa tarehe 9 Novemba baada ya kuzuiliwa kwa siku 12.

Diaz alikosa mechi mbili za klabu katika kipindi hicho lakini aliunganishwa tena na Luis Manuel Diaz siku ya Jumanne na akaifungia nchi yake mabao mawili dhidi ya Brazil siku ya Alhamisi, huku baba yake akitazama akiwa jukwaani.

Hata kukiwa na matokeo chanya, Mikel anaamini utekaji nyara kama huo unaweza kuacha alama za kudumu na za kina kwenye ustawi wa kiakili na kihisia wa mchezaji.

"Tajriba ya aina hii haikuachi, hata baada ya wapendwa wako kurudi nyumbani," Mikel aliiambia BBC Sport Africa.

"Ni bahati mbaya sisi ni walengwa. Ni hali ngumu kwa mtu yeyote kustahimili na natumai hakuna mtu atakayeipitia."

Mnamo 2011 babake Mikel, Pa Michael Obi, alivumilia muda wa siku kumi kizuizini kabla ya kuachiliwa. Kisha alitekwa nyara tena mnamo 2018, na Mikel aligundua wakati akijiandaa kuichezea Nigeria dhidi ya Argentina kwenye Kombe la Dunia nchini Urusi.

"Baba yangu alitekwa nyara dakika chache kabla ya mchezo mmoja mkubwa zaidi wa maisha yangu.

"Alitishwa na nilikosa utulivu kihisia nilipokuwa nikicheza uwanjani. Ilikuwa ni hali ya kutisha sana kwangu.

"Ni hali ambayo hujisikii kabisa."

Mikel amesisitiza haja ya klabu za kandanda, mashirika na mabaraza tawala kuweka kipaumbele afya ya akili na ustawi wa jumla wa wachezaji wanaokabiliana na hali kama hizo za kiwewe, na kuwahimiza wanasoka na familia zao kutafuta usaidizi wa kitaalamu na usaidizi wakati wa dhiki.

Chelsea ndio timu bora' kwa Osimhen

Mshambuliaji wa Napoli na Nigeria Victor Osimhen alikuwa mchezaji wa hivi karibuni , akifichua kuwa alikataa uwezekano wa kuhamia Saudi Arabia mapema mwaka huu kwa ajili ya "kulinda kazi yake".

Mikel anasema "ingekuwa ndoto" kucheza na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, mgombea aliye kifua mbele kuwania tuzo ya Mwanasoka Bora wa Afrika ambaye alikuwa mfungaji bora wa Serie A ya Italia mwaka jana huku Napoli ikishinda taji la kwanza baada ya miaka 33. .

Na Mikel anataka Osimhen ahamie London ili kujiunga na klabu yake ya zamani, ambako anaamini ana uwezo wa kuiga mafanikio yaliyofikiwa na mshambuliaji maarufu wa Ivory Coast Didier Drogba huko Stamford Bridge.

"Kipaji chake, ari ya kupigana ni dhahiri," Mikel alisema.

"Didier Drogba alikuwa na mchezo mzuri Stamford Bridge. Osimhen, kama Mwafrika, anaweza kuendelea katika njia hiyo.

"Chelsea ni hatua nzuri kwa Victor Osimhen kuendelea na uchezaji wake."