Mshambulizi wa zamani wa Liverpool Roberto Firmino afiwa na babake

Mzee huyo mwenye umri wa miaka 62 alifariki akiwa safarini na familia yake kueleka Dubai.

Muhtasari

• Marafiki wa karibu na meneja wa vyombo vya habari wa Firmino wamethibitisha habari hiyo kwa chombo cha habari cha Brazil UOL.

Roberto Firmino afiwa na babake
Roberto Firmino afiwa na babake
Image: Hisani, Instagram

Babake mchezaji wa zamani wa Liverpool, Roberto Firmino aliaga dunia Jumamosi usiku wakati wa safari ya familia kwenda Dubai.

José Roberto Cordeiro de Oliveira, 62, alipata mshtuko wa moyo.

Familia bado inajaribu kuwasiliana na ubalozi wa Brazil nchini ili kurudisha mwili wake Maceió, mji wa nyumbani wa familia hiyo.

Marafiki wa karibu na meneja wa vyombo vya habari wa Firmino wamethibitisha habari hiyo kwa chombo cha habari cha Brazil UOL.

'Alikuwa mtu mzuri sana,' akasema rafiki mmoja wa familia hiyo. 'Alikuwa na roho nzuri sana na alikuwa mcheshi sana. Hili halikutarajiwa sana.'

Firmino alimwona baba yake kama shujaa, kama alivyoandika katika wasifu wake 'Si Señor - Miaka Yangu ya Liverpool'.

'Sio mashujaa wote huvaa kofia; wengine wanaitwa Baba. Baba yangu, José, alikuwa shujaa wangu wa utotoni, msukumo na mfano mzuri. Mwanaume mkarimu, mkweli, mwaminifu aliyejitolea kwa familia.'

Larissa Pereira, mke wa Firmino, alichapisha baadhi ya picha na video akiwa na baba mkwe wake. 'Asante kwa wakati huu, Baba', aliandika.

CRB, klabu ya kwanza ya Firmino, pia iliandika ujumbe kwa José Cordeiro, ambaye alifurahi sana kuona mtoto wake akicheza huko.