Sehemu ya dari ya Old Trafford inasemekana iliwaangusha mashabiki mnamo Novemba 19 wakati Wanawake wa Manchester United wakiwakaribisha wapinzani wao wa jiji la Manchester City.
Hali mbaya ya uwanja huo imeangaziwa siku za nyuma, huku umiliki wa sasa wa familia ya Glazers ukishutumiwa kwa kutowekeza katika ukarabati wake.
Mtumiaji wa X (zamani Twitter), Problemchild, alidai kuwa:
"Ikiwa utahitaji uthibitisho zaidi kwamba Old Trafford inaanguka ... Sehemu za dari za Block N2402 ziliangukia wafuasi 2 kwenye mchezo wa wanawake leo."
Wiki kadhaa nyuma, kanda nyingine iliibuka mtandaoni ya paa zikivuja huku mvua ikiendelea kunyesha sehemu kadhaa za Uingereza.
Kama gazeti la Mirror linavyoripoti, uwanja huo unaokalia watu 75,000 umepoteza sura yake nzuri katika miaka ya hivi karibuni. Hivi majuzi ulipuuzwa kama moja ya uwanja wa mwenyeji wa Euro 2028, huku Etihad ikichaguliwa kama uwanja wenye makao yake mjini Manchester.
Mashabiki wa Manchester United wamekuwa wakizozana mara kadhaa, wakipinga familia ya Glazers, ambayo wanaituhumu kwa kupuuza mahitaji ya klabu hiyo.
Mashetani Wekundu wamekwama tangu Sir Alex Ferguson alipoondoka mwaka wa 2013, huku pesa zikimwagika kwa walengwa ambao walishindwa kutimiza uwezo wao.
Kwa muda mrefu kumekuwa na makabiliano makali ya maneno kutoka kwa mashabiki ambao mara si moja wamekuwa wakiinua mabango ya kuitaka familia ya Glazera kuachilia uongozi wa timu hiyo kwa kuuza hisa zake.
Hivi majuzi, tajiri kutoka Qatari, Sheikh Jassim alijiondoa katika mpango wa kununua klabu hiyo baada ya kunyimwa nafasi ya kununua hisa zote.
Kwa mujibu wa taarifa, Sheikh Jassim aliambiwa anunue asilimia Fulani ya hisa wakati yeye alitaka kupewa hisa zote.
Kujiondoa kwake kulivutia hasira Zaidi kutoka kwa mashabiki ambao walihisi uongozi wa timu ungefufuka mikononi mwa Jassim.