Klabu ya soka Uingereza yamfuta kocha kwa kupoteza mechi 3 tu ndani ya mechi 14

Mkufunzi huyo mwenye umri wa miaka 39, ambaye amekuwa mchezaji/meneja katika klabuni kwa miaka saba, ameiwezesha timu yake kushinda mara 10 katika mechi 14 msimu huu

Muhtasari

• Timu hiyo inashika nafasi ya pili kwenye jedwali la Ligi Daraja la Kwanza la Ligi ya Magharibi, pointi moja tu nyuma ya viongozi Helston Athletic.

Mpira
Mpira
Image: EPL//FACEBOOK

Klabu ya daraja la tisa nchini Uongereza, Bridgwater United imekosolewa vikali kwa kauli yao ya "maneno mabaya" na "ya kufedhehesha" kuthibitisha kufutwa kazi kwa kocha wa muda mrefu, Dave Pearse.

Pearse aliondolewa majukumu yake Jumatatu alasiri kufuatia kichapo cha 2-1 cha timu yake kwenye Torpoint Athletic, Sportbible wameripoti.

Lakini wengi wametilia shaka uamuzi huo wa mshangao kwani Bridgwater iliye katika fomu inashika nafasi ya pili kwenye jedwali la Ligi Daraja la Kwanza la Ligi ya Magharibi, pointi moja tu nyuma ya viongozi Helston Athletic.

Mkufunzi huyo mwenye umri wa miaka 39, ambaye amekuwa mchezaji/meneja katika klabu ya Bridgwater kwa miaka saba, ameiwezesha timu yake kushinda mara 10 katika mechi 14 msimu huu.

Hayo yamesemwa, klabu imehamia kumpandisha cheo meneja wao msaidizi, Andy Llewellyn, kama bosi wa muda kabla ya pambano lao lijalo dhidi ya Nailsea & Tickenham.

Katika taarifa kwenye akaunti yao rasmi ya X, Bridgwater walithibitisha kufukuzwa kwa Pearse.

"Klabu inatangaza kwamba Dave Pearse meneja wa klabu ameondoka Bridgwater United," waliandika.

"Baada ya miaka 7 kama Mchezaji na Meneja (miaka 2 ya mapumziko ya covid) klabu haijapanda daraja. Matokeo ya msimu huu hadi sasa yamekuwa mazuri lakini si makubwa. Hasara 3 zilizoigharimu klabu pointi 9 na gharama ya zaidi ya £10k ni haikubaliki kwa mmiliki wetu mpya Ian Davis.”

"Ian ni shabiki mkubwa wa soka na anataka klabu ipandishwe daraja na amefanya uamuzi huu kwa moyo mzito lakini anahisi ni muhimu sana damu mpya itambulishwe kwa klabu ili kuipa nguvu inayohitaji kwa sasa.”

"Ian amewekeza kiasi kikubwa ili kuiondoa klabu katika madeni na ameboresha misingi na vifaa na anataka tu kile ambacho ni bora kwa klabu. Yote yanahusu klabu si mtu yeyote."

Hata hivyo, maneno haya makali ya kumfuta kocha kufuatia kupoteza mechi 3 pekee kati ya 14 na pia kudai uamuzi wa kumfuta unachochewa na hasara na pauni elfu 10 pekee yamezua hasira miongoni mwa mashabiki.

Hivi ndivyo mitandao ya kijamii iliitikia kauli hiyo.

Shabiki mmoja alisema: "Yote kwa yote, ni taarifa ya maneno ya kutisha. Hakuna zaidi ya mchezo usioeleweka. Kisha unagundua kuwa wao ni wa 2 kwa kushindwa mara 3 tu kati ya 14, pamoja na kuzingatia utumishi wa muda mrefu wa meneja na jambo zima hata zaidi lintatanisha."

Wa pili aliandika: "Wa pili kwenye ligi, wakiwa juu hadi wikendi iliyopita. Unataka 'damu safi' lakini mpandishe meneja msaidizi. Haya ni mambo sahihi ya aina ya Harchester United. Ludicrous."