Pochettino athibitisha Nkunku kucheza mechi ya kwanza ya msimu wikendi hii

Safu ya ushambulizi ya Chelsea imekuwa ikisuasua kwa ubutu huku Nicolas Jackson na Armando Broja wakionekana kukosa kumakinika mbele ya lango licha ya kuandaliwa mipira mingi kutoka safu ya kati.

Muhtasari

• Pochettino pia alikiri kumpoteza Sanchez kutakuwa pigo kwa timu, kwani kumkosa kipa wako wa kawaida kwa muda bila shaka itakuwa ngumu.

• Akizungumza na wanahabari mbele ya mechi yao dhidi ya Sheffied United iliyopo mkiani, Pochettino alisema kwamba mshambulizi huyo atakuwa kikosini.

Nkuku.
Nkuku.
Image: Facebook

Kocha wa Chelsea Mauricio Pochettino amethibitisha kwamba mshambulizi mpya wa timu hiyo Christopher Nkuku atajumuishwa kwenye kikosi kwa mara ya kwanza tangu kusajiliwa  simu wa joto, wikendi hii.

Nkuku alipata jeraha baya wakati wa mechi za kujifua kuelekea msimu mpya na tangia hapo maekuwa akiuguza jeraha nje ya uwanja wakati Chelsea wamekuwa wakitaabika kusaka mabao na safu yao butu ya ushambuliaji ikiongozwa na Nicolas Jackson na Armando Broja.

Akizungumza na wanahabari mbele ya mechi yao dhidi ya Sheffied United iliyopo mkiani, Pochettino alisema kwamba mshambulizi huyo atakuwa kikosini.

‘Anaweza kuhusika. Hiyo ni habari njema sana kwetu kwa sababu akihusika kesho na kuwa kikosini, anaweza kuanza kuhisi ushindani, kuhisi Ligi Kuu, na kuwa na wachezaji wenzake kwa mara ya kwanza baada ya pre-season.’

"Sasa tunahitaji kuwa watulivu na watulivu kwa sababu hatutaki kuweka shinikizo zote kwake. Sasa anahitaji kubadilika, kujua Ligi Kuu, kujua ushindani. Lakini ni motisha kubwa pia kwetu, kwa wachezaji wenzake na kwa mashabiki wetu kuona mchezaji ambaye anafaa kuwa muhimu kwetu kikosini kwa mara ya kwanza msimu huu.’

Pochettino pia alikiri kumpoteza Sanchez kutakuwa pigo kwa timu, kwani kumkosa kipa wako wa kawaida kwa muda bila shaka itakuwa ngumu.

 

‘Utaumia kila mara unapokuwa na jeraha kwa mchezaji ambaye amekuwa kipa wetu namba moja hadi sasa, huwa ni mchezaji ambaye utamkosa. Lakini tuna mlinzi mwingine ambaye amekuwa akifanya kazi kwa bidii ili kuwa tayari ikiwa aina hii ya kitu kitatokea.

 

"Kwa kweli, nina huzuni sana kwa sababu tutapoteza mchezaji labda kwa wiki chache. Bado tunahitaji kusubiri na kuona kikamilifu hali ilivyo na Robert, lakini pia na Reece na Marc. Nadhani tangu mwanzo tunakumbwa na mazingira tofauti. Hii ni hali muhimu lakini tunatakiwa kuwa na nguvu kwa sababu ushindani haukomi na tunatakiwa kuwa tayari kushindana.’