Fahamu njia sahihi ya kutamka majina magumu ya wachezaji wa EPL

Tazama orodha kamili ya wachezaji waliofichua matamshi sahihi ya majina yao.

Muhtasari

•Baadhi ya wachezaji mashuhuri wa EPL wenye majina ya kutatanisha walitengeneza video inayoonyesha jinsi yanavyotakiwa kutamkwa.

•Wachezaji hao ni pamoja na Kevin De Bruyne, Dominic Szoboszlai , Mykhailo Mudryk, Josko Gvardiol, Pep Guardiola miongoni mwa wengine.

Baadhi ya wachezaji wa EPL wenye majina magumu.
Image: HISANI

Hivi majuzi, baadhi ya wachezaji mashuhuri wa Ligi Kuu ya Uingereza  (EPL) wenye majina ya kutatanisha walitengeneza video inayoonyesha jinsi yanavyotakiwa kutamkwa.

Wachezaji na mameneja zaidi ya 30 kutoka vilabu tofauti katika EPL walionekana kwenye video hiyo ambayo ilishirikiwa kwenye akaunti rasmi za ligi hiyo maarufu.

Hatua hiyo ililenga kuwasaidia mashabiki wa soka kote duniani kujua matamshi sahihi ya majina ya wachezaji wanaowapenda wenye majina magumu sana. Wachezaji hao ni pamoja na Kevin De Bruyne, Dominic Szoboszlai , Mykhailo Mudryk, Josko Gvardiol, Pep Guardiola miongoni mwa wengine.

Tazama orodha kamili ya wachezaji waliofichua matamshi sahihi ya majina yao;-

1. Dominic Szoboszlai (Liverpool) : Do-min-ik Sob-oss-lye

2. Josko Gvardiol (Man City) : Yosh-Ko Vardy-ol

3. Rasmus Hojlund (Man United) : Razz-mus Hoy-lun

4. Dejan Kulusevski (Tottenham) : Day-yan Ku-loo-sev-ski

5. Mykhailo Mudryk (Chelsea) : Me-kyle-o Moo-drick

6. Bruno Guimaraes (Newcastle) : Bru-no Gi-ma-rays

7. Facundo Buonanotte (Brighton) : Fa-cun-do Bwena-not-ay

8. Kevin De Bruyne (Man City : Kev-in De Bruh-ner

9. Bruno Fernandes (Man United) : Bru-no Mig-el borj Fer-nanj

10. Jakub Kiwior (Arsenal) : Ya-kub Key-vee-or

11. Kaoru Mitoma (Brighton) : Kar Me-toe-ma

12. Alejandro Garnacho (Man U) : Al-handro har-na-cho

13. Tomas Soucek (West Ham) : Tomaj So-check

14. Bryan Mbeumo (Brentford) :  Bry-an Ber-mo

15. Anel Ahmedhodzic (Sheffield United)  : An-el Ar-med-hod-ich

16. Sasa Kalajdzic (Wolves)  : Sasha Ka-liez-itch

17. Nayef Aguerd (West Ham)  : Nye-ef Agg-erd

18. Stefan Bajcetic (Liverpool)  : Stefan bye-chet-itch

19. Illia Zabarnyi (Bournemouth) :  Ill-iya  Za-bar-ney

20. Femi Seriki (Sheffield United)  : Fem-ee  Ser-iki

21. Joao Palhinha (Fulham) :  Joo-wow  Pow-lee-nia

22. Chiedozie Ogbene (Luton Town) : Chi-do-zay  Og-ben-eh

23. Jili Buyabu (Sheffield United)  : Ji-lee  Boo-ya-bu

24. Noni Madueke (Chelsea) : No-ni  Mad-way-kay

25. Benie Traore (Sheffield United) : Benny Ad-am-ah  Try-or-ray

26. Kebin Schade (Brentford) : Kev-in Shade

27. Thiago Alcantara (Liverpool) : Tee-aa-gow  Al-kan-taa-ruh

28.Fabian Schar (Newcastle) : Fa-bian Share

29.Moussa Niakhate (Nottingham Forest) : Moo-sa Nia-kat-ay

30. Caoimhin Kelleher (Liverpool) : Kee-veen Kell-le-her

31. Yasser Larouci (Sheffield United) : Yes-are La-roos

32. Issa Kabore (Luton Town) : Is-a Kab-or-ray

33. Facundo Pellistri (Man United) : Fa-cun-doh Pel-is-tree

34.Bart Verbruggen (Brighton) : Bart Ver-bruh-hen

35. Yehor Yarmolyuk (Brentford) : Ye-hor Yar-mo-luk

36. Andoni Iraola (Bournemouth) : An-doni Iyar-ola

37. Pep Guardiola ( Man City) : Pep Gwar-dee-ola

HISANI: PREMIER LEAGUE