Mo Salah awa mchezaji wa 5 kufunga mabao 150+ kwa klabu moja katika EPL

Mo Salah aliingia kweney safu hii ya kipekee akijiunga na wenzake kama Thierry Henry, Sergio Aguero, Wyne Rooney na Harry Kane.

Muhtasari

• Katika mechi hiyo ngumu, Liverpool walishinda mabao 4-2 na kusisima nafasi yao kileleni mwa jedwali.

Mohamed Salah
Mohamed Salah
Image: Facebook

Winga matata wa Liverpool na timu ya taifa ya Misri, Mohamed Salah amekuwa mchezaji wa tano kufungia klabu moja mabao Zaidi ya 150 katika ligi kuu ya EPL nchini Uingereza.

Mo Salah alifanikisha rekodi hii wiki moja tu kuelekea mashindano ya bara la Afrika, AFCON nchini Ivroty Coast ambapo alifunga mabao 2 katika mtanange wao mkali dhidi ya Newcastle.

Katika mechi hiyo ngumu, Liverpool walishinda mabao 4-2 na kusisima nafasi yao kileleni mwa jedwali.

Ligi ya EPL inajulikana kama ligi yenye ushindani mkubwa na hilo linaweza kuonekana wazi kwa uchache wa wachezaji ambao waliwahi kufunga mabao Zaidi ya 150 wakiwa wanachezea timu moja tu kwenye ligi.

Kando na Mo Salah, wachezaji wengine ambao wako katika safu hiyo ya kipekee ni pamoja na nahodha wa timu ya taifa ya Uingereza, Harry Kane ambaye aliondoka Tttenham mwanzoni mwa msimu huu  baada ya kuitumikia kwa muda mrefu.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 pia aliacha matokeo ya kudumu upande, akifunga mabao 278 katika mashindano yote kwao.

Ilikuwa kwenye Premier League ambapo Kane aling'ara sana, akifunga mabao 213 katika mechi 317, akiwa pia mfungaji bora wa muda wote wa Tottenham.

Mchezaji mwingine ni aliyekuwa mshambulizi wa Manchester City Sergio Aguero ambaye alifunga mabao 260 katika michuano yote 390 aliyowajibikia City.

katika Ligi ya Premia, Aguero alifunga mabao 185 kabla ya kuondoka katika klabu hiyo mwaka wa 2021.

Mshambulizi Muingereza Wayne Rooney alifunga mabao 208 kwenye Premier League, lakini si yote yaliyofungwa kwa klabu moja.

Meneja wa sasa wa Birmingham City aliifungia Everton mara 25 kabla ya kuhamia Manchester United.

Ilikuwa ni kwa Mashetani Wekundu ambapo Rooney alifanya vyema, kwani alifunga mabao 183 katika michezo 393 kwenye ligi pekee.

Thierry Henry alikua gwiji katika Klabu ya Soka ya Arsenal.

Mfaransa huyo alishinda ligi mara mbili na timu hiyo na Kombe la FA mara tatu na alifunga mabao 228 kwa upande katika mashindano yote.

Katika EPL, Henry alifunga mabao mengi 175 katika michezo 258, Transfermarkt ilibaini.