Mchezaji wa Inter adondokwa na suruali akisherehekea kufunga bao dakika za mazidadi

Baada ya Frattesi kufunga bao kunako dakika za zima taa tulale, alikimbia uwanjani na kusherehekea kwa mtindo wa mbwembwe huku suruali yake ikimdondoka na kumuacha makalio uchi.

Muhtasari

• Hata hivyo, mechi hiyo ilikamilika kwa kivumbi na kitivutivu cha aina yake baada ya Verona pia kukosa kufunga mkwaju wa penati kunako dakika ya 100.

Davide Frattesi
Davide Frattesi
Image: x

Kisa cha kushangaza kilishuhudiwa usiku wa Jumamosi katika mechi ya kufana baina ya Inter Milan na Hellas Verona katika ligi kuu ya nchini Italia.

Inter walifunga katika dakika ya nne ya muda wa nyongeza katika kumaliza kwa fujo San Siro, huku bao la kiungo wa kati Davide Frattesi likiwaweka mbele kwa pointi tano kileleni mwa jedwali.

Hata hivyo, mechi hiyo ilikamilika kwa kivumbi na kitivutivu cha aina yake baada ya Verona pia kukosa kufunga mkwaju wa penati kunako dakika ya 100.

Sports Brief wanaripoti kwamba Lautaro Martinez alikuwa ameipatia timu yake bao la kuongoza katika kipindi cha kwanza, akiuwahi mpira kutoka kwa Henrikh Mkhitaryan na kuipiga timu yake mbele.

Mabadiliko ya Verona katika kipindi cha pili yalizaa matunda, Thomas Henry alipata bao la kusawazisha kwa kuunganisha krosi ya Duda dakika moja tu baada ya kuingia.

Mchezo ulionekana kuelekea sare ya kutatanisha kwa Inter, lakini upande wa Simeone Inzaghi walisonga mbele, mwishowe wakazaa matunda.

Baada ya Frattesi kufunga bao kunako dakika za zima taa tulale, alikimbia uwanjani na kusherehekea kwa mtindo wa mbwembwe huku suruali yake ikimdondoka na kumuacha makalio uchi.

Baada ya kugeuza mpira ndani, kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24 alikimbia hadi kwenye uzio, akiwatenganisha mashabiki na shimo, akijaribu kuuruka.

Akiwa na furaha tele, alishindwa kuvuka na kuanza kushangilia kutoka kwenye uzio, huku wenzake wakijumuika mara baada ya hapo.

Video za sherehe hizo zimekumba mitandao ya kijamii huku wachezaji wa Inter wakikaribia kumvua nguo mshindi wa mechi yao katika msisimko wote. Tukio zima lilikuwa la kuvutia kutazama.