Mwanasoka wa Israel akamatwa baada ya ku'dedicate bao kwa waliotekwa nyara na Hamas

Jehezkel, 28, alishikilia ngumi yake iliyokunjwa juu kuonyesha ujumbe huo baada ya kuifungia bao timu yake.

Muhtasari

• Vyombo vya habari vya Uturuki viliripoti kwamba bosi wa klabu yake, Sinan Boztepe, alimfuta kazi na kusema: 'Maadili yetu ya kitaifa ni juu ya yote. Haijalishi mchezaji ataleta kiasi gani kwenye klabu. Tutasitisha mkataba wake.'

 

Sagiv Jehezkel, mchezaji wa Israeli
Sagiv Jehezkel, mchezaji wa Israeli
Image: X

Mchezaji wa kandanda wa Israel amekamatwa na kufukuzwa kazi katika klabu yake nchini Uturuki na kufukuzwa nchini humo baada ya kulitoa goli kwa mateka waliotekwa na Hamas zaidi ya siku 100 zilizopita siku ya Black Saturday, Daily Online wameripoti.

Polisi wa Uturuki walimzuilia mchezaji wa Israel Sagiv Jehezkel na kumhoji Jumatatu juu ya ujumbe aliouweka kwenye kifundo cha mkono wake wakati wa mechi ya daraja la juu iliyorejelea kupita siku 100 tangu shambulio la Hamas la Oktoba 7 nchini Israel, vyombo vya habari vya serikali vilisema.

Waziri wa Sheria wa Uturuki Yilmaz Tunc alisema waendesha mashtaka walikuwa wanamchunguza Jehezkel kwa shtaka la 'kuchochea watu kwenye chuki na uadui' kwa kuonyesha barua iliyoandikwa kwenye kiganja chake chenye bandeji ikisema 'siku 100, 7.10', pamoja na nembo ya Nyota ya Kiyahudi ya Daudi.

Jehezkel, 28, alishikilia ngumi yake iliyokunjwa juu kuonyesha ujumbe huo baada ya kuifungia bao timu yake, klabu ya Antalyaspor ya kusini mwa Uturuki, dhidi ya Trabzonspor kwenye Super Lig ya Uturuki siku ya Jumapili.

Jehezkel ameachiliwa akisubiri kusikilizwa kwa kesi yake, na vyombo vya habari vya Israel viliripoti kuwa ndege ya kibinafsi imetumwa kutoka Israel kumchukua yeye na familia yake ili waweze kumrudisha nyumbani.

Vyombo vya habari vya Uturuki viliripoti kwamba bosi wa klabu yake, Sinan Boztepe, alimfuta kazi na kusema: 'Maadili yetu ya kitaifa ni juu ya yote. Haijalishi mchezaji ataleta kiasi gani kwenye klabu. Tutasitisha mkataba wake.'

Waendesha mashtaka wa Antalya walianzisha uchunguzi dhidi ya Jehezkel 'kutokana na kitendo chake cha kuunga mkono mauaji ya Israel huko Gaza baada ya kufunga bao' Tunc alisema kwenye mtandao wa kijamii wa X.