Video ya kuchukiza ya beki wa Arsenal akibusiana na mbwa kimahaba yazua hisia mseto (+video)

Beki wa Arsenal, Nuno Tavares amekuwa akivuma kwa sababu zisizo sahihi siku ya Jumatatu asubuhi.

Muhtasari

•Video ya Tavares akiwa na wakati wa kimapenzi na mbwa wake zimesambazwa mitandaoni na kuzua mjadala mkali, hisia mseto na ukosoaji mkubwa.

•Watumiaji wengi wa X wameendelea kutoa maoni yao kuhusu kitendo cha beki huyo mwenye umri wa miaka 23 huku wengi wakionekana kushtuka.

akibusu na mbwa kimahaba imezua hisia mseto mitandaoni.
Video ya Nuno Tavares akibusu na mbwa kimahaba imezua hisia mseto mitandaoni.
Image: HISANI

Beki wa kushoto wa Arsenal ambaye yuko kwa mkopo Nottingham Forest, Nuno Tavares amekuwa akivuma kwa sababu zisizo sahihi siku ya Jumatatu asubuhi.

Video za mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno mwenye umri wa miaka 23 akiwa na wakati wa kimapenzi na mbwa wake zimesambazwa kwenye mitandao ya kijamii na kuzua mjadala mkali, hisia mseto na ukosoaji mkubwa.

Katika mojawapo ya video hizo, beki huyo wa kushoto alionekana akifungua midomo yake ili mbwa mweupe ailambe. Video nyingine pia inawaonyesha mbwa wawili wakilamba mdomo wake ulio wazi huku akionekana kufurahia sana kitendo hicho.

Nia ya Nuno Tavares bado haijabainika wazi lakini video hiyo hakika imefanya watu watilie shaka uhusiano wake na mbwa wake. Watumiaji wengi wa mtandao wa X wameendelea kutoa maoni yao kuhusu kitendo cha beki huyo mwenye umri wa miaka 23 huku wengi wakionekana kushtuka.

Tazama maoni ya baadhi ya watumizi wa mtandao wa X;

@ukemerinho: Video ya Nuno Tavares inachukiza sana 🤮. Tafadhali akirudi London Colney, mweke Win (mbwa wetu wa mafunzo) mbali naye.

@AFC_Chlo: Nimeamka tu nakuona video hiyo ya Nuno Tavares, tayari imeharibu siku yangu 😭

@La_esterisco: Nuno Tavares anafanya nini kusema kweli??

@rebekkarnold: Video hiyo ya Nuno Tavares ilikuwa kitu ambacho sikuhitaji kuona kabla ya 9am siku ya Jumatatu asubuhi.

@Yourchargie: Nuno Tavares wewe ni aibu kwa ulimwengu.

@chipashachangal: Video hiyo ya Nuno Tavares inasumbua sana.