Lampard ataja makocha 2 ambao Abrahamovic alikosea kuwafuta kazi Chelsea

Lampard ni mmoja wa wachezaji waliochezea Chelsea kwa muda mrefu – miaka 13, miaka 11 ikiwa ni chini ya Mrusi huyo.

Muhtasari

• Abrahamovic aliimiliki Chelsea kwa miaka 19 kabla ya kushurutishwa kuipiga mnada mwaka 2022.

• Lampard ni mmoja wa wachezaji waliochezea Chelsea kwa muda mrefu – miaka 13, miaka 11 ikiwa ni chini ya Mrusi huyo.

Frank Lampard, Lejendari ya klabu ya Chelsea
Frank Lampard, Lejendari ya klabu ya Chelsea
Image: Screengrab//YouTube

Mchezaji wa zamani wa Chelsea ambaye pia aliifunza timu hiyo, Frank Lampard amefichua makocha wawili ambao anahisi mmiliki wa zamani wa klabu, Roman Abrahamovic alikosea kuwafuta kazi.

Akizungmza katika podikasti ya Stick to Football, Lampard alisema anahisi mmiliki huyo wa zamani raia wa Urusi wakati mwingine alikuwa anakosa subira na kufanya maamuzi mabaya.

Abrahamovic aliimiliki Chelsea kwa miaka 19 kabla ya kushurutishwa kuipiga mnada mwaka 2022.

Lampard ni mmoja wa wachezaji waliochezea Chelsea kwa muda mrefu – miaka 13, miaka 11 ikiwa ni chini ya Mrusi huyo.

Muingereza huyo alisema kwamba Abrahamovic alikosea kuwafuta kazi makocha Jose Mourinho wa Ureno na Muitaliano Carlo Ancelotti.

"Sijui ni kwa kiasi gani [mambo yangekuwa tofauti], ikiwa [Roman Abramovich] angeshikamana na Jose [Mourinho] kupitia sehemu hiyo [mbaya] na angeendelea," alisema.

"Najua historia ya Jose sasa inaonekana kama anaendelea baada ya miaka michache, kisha Carlo [Ancelotti] akaondoka baada ya miaka miwili - mameneja wazuri wa kiwango cha juu."

Mfungaji bora wa muda wote wa klabu hiyo pia alikuwa mwathiriwa wa sera ya kuajiri na kuachishwa kazi alipoisimamia klabu hiyo kuanzia Julai 2019 hadi alipotimuliwa Januari 2021 baada ya matokeo mabaya.

Mrithi wake, Thomas Tuchel, aliichukua timu hiyo kutoka nafasi ya 9, na kutinga nne bora na kushinda kombe la pili la UEFA Champions League ndani ya miezi minne.