Haller aipa Ivory Coast ushindi katika fainali ya Afcon

Wenyeji hao wa Afrika Magharibi waliongeza ushindi wao wa awali wa Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 1992 na 2015.

Muhtasari

•Sebastien Haller alikuwa shujaa wa Ivory Coast tena wakati The Elephants walipotoka nyuma na kuwashinda Nigeria mabao 2-1 .

•The Elephants wanachukua $7m (£5.54m) kama pesa za zawadi, huku Nigeria ikikabidhiwa $4m na Shirikisho la Soka Afrika.

Image: BBC

Sebastien Haller alikuwa shujaa wa Ivory Coast tena wakati The Elephants walipotoka nyuma na kuwashinda Nigeria mabao 2-1 na kushinda fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2023 wakiwa nyumbani .

Mshambulizi huyo, ambaye pia alifunga bao la ushindi wa nusu fainali miezi 13 tu tangu arejee kutoka matibabu ya saratani ya tezi dume,aliunganisha krosi ya Simon Adingra na kidole cha guu la kiatu chake zikiwa zimesalia dakika tisa kukamilisha mchezo huo kipindi cha pili na kuibua shangwe kali jijini Abidjan.

William Troost-Ekong alikuwa ameiweka Nigeria mbele dakika saba kabla ya kumalizika kwa kipindi cha kwanza wakati beki huyo wa kati alipopanda juu zaidi na kufunga kwa kichwa kutoka umbali wa yadi tisa kufuatia kona.

Franck Kessie alifunga bao la kusawazisha dakika ya 62 baada ya kuachwa bila kuthibitiwa kwenye lango la nyuma kutokana na kona ya Adingra.

Baada ya kukimbia kwa kasi hadi fainali, ambayo ni pamoja na kuondoka kwa kocha Jean-Louis Gasset baada ya kushindwa mara mbili katika hatua ya makundi, Ivory Coast walinyakua taji la tatu la bara na ushindi waliosatahili kuupata .

Wenyeji hao wa Afrika Magharibi waliongeza ushindi wao wa awali wa Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 1992 na 2015 na kuwa waandaji wa kwanza wa michuano hiyo kushinda tangu Misri ilipotwaa kombe hilo mwaka wa 2006.

Kocha wa muda Emerse Fae ndiye aliyepanga Ivory Coast kupita hatua ya muondoano, ambayo ilijumuisha ushindi mnono dhidi ya mabingwa watetezi Senegal na Mali baada ya kusawazisha dakika za lala salama katika michezo yote miwili.

Ivory Coast ilitumia zaidi ya $1bn (£0.79bn) kuandaa michuano hiyo,ikiwekeza kiasi sawa na hicho katika kuboresha miundombinu nchini humo, na Rais wa Ivory Coast Alassane Outtara alijiunga na sherehe za baada ya mechi katika uwanja huo uliopewa jina lake.

The Elephants wanachukua $7m (£5.54m) kama pesa za zawadi, huku Nigeria ikikabidhiwa $4m na Shirikisho la Soka Afrika.