Emilio Nsue: Mfungaji bora wa AFCON atimuliwa nje ya timu ya taifa kisa dai la ufisadi

Nsue, ambaye aliibuka mfungaji bora wa AFCON 2023 akiwa na mabao matano, amefichua ubadhirifu wa fedha ndani ya shirikisho hilo.

Muhtasari

• Nsue, ambaye aliibuka mfungaji bora wa AFCON 2023 akiwa na mabao matano, amefichua ubadhirifu wa fedha ndani ya shirikisho hilo.

Nsue
Nsue
Image: Instagram

Mshambulizi wa timu ya taifa la Equatorial Guinea, Emilio Nsue na mwenzake Edu Salvador wamefukuzwa nje ya timu ya taifa kutokana na "matukio mengi ya utovu wa nidhamu" kwa mchezaji huyo wa zamani na kuhusika "katika tukio lisilo la kufurahisha huko Abidjan" kwa timu hiyo wakati wa kipute cha AFCON.

Katika taarifa iliyotolewa Jumanne Februari 13, 2024, siku mbili baada ya fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika iliyoshinda Ivory Coast, Shirikisho la Soka la Equatoguinean (FEGUIFUT) limewasimamisha Emilio Nsue Lopez na Ivan Salvador kuichezea timu ya taifa hadi itakapotangazwa tena.

Ingawa maelezo ya kutengwa haya hayajabainika, taarifa hiyo inaeleza kuwa Nsue atawajibika kwa "matukio kadhaa ya utovu wa nidhamu, kabla na baada ya ushiriki wa timu yake ya taifa katika toleo la 34 la Kombe la Mataifa ya Afrika."

Hivi majuzi alikuwa ameshinda taji la heshima la mfungaji bora wa shindano hilo na mabao yake matano aliyafunga wakati wa michuano hiyo, yakiwemo mawili dhidi ya Ivory Coast katika hatua ya makundi (0-4).

Baada ya tangazo la kufukuzwa kwa timu ya taifa, Nsue kupitia Instagram live yake alitoa madai kadha wa kadha dhidi ya shirikisho la soka la Equatorial Guinea, FEGUIFUT akisema kwamba shirikisho hilo lilivuja pesa kadhaa zilizokusudiwa kuwasaidia wachezaji katika Afcon.

Nsue, ambaye aliibuka mfungaji bora wa AFCON 2023 akiwa na mabao matano, amefichua ubadhirifu wa fedha ndani ya shirikisho hilo.

Anadai kuwa zaidi ya Euro milioni 1 (Ksh154,983,600) kutokana na mapato ya mashindano hayo bado hayajulikani yalipo, na hivyo kutoa picha mbaya ya kupuuzwa na unyonyaji.

Mshambuliaji huyo alisimulia jinsi wachezaji walivyolazimika kujilipia vifaa vyao na kueleza kwa kina kitendo cha shirikisho hilo kushindwa kuwalipa madeni watoa huduma ikiwemo hoteli.