Kylian Mbappe amekubali mkataba wa kujiunga na Real Madrid msimu huu wa joto

Meneja wa Real Carlo Ancelotti tayari amefikiria jinsi atakavyomtumia Mbappe katika timu yake

Muhtasari
  • Nahodha huyo wa Ufaransa, 25, ameiambia PSG kuwa ana nia ya kuondoka klabu hiyo huku kandarasi yake ikikamilika mwezi Juni.
Mbappe akanusha kutaka kuondoka PSG
Mbappe akanusha kutaka kuondoka PSG
Image: Maktaba

Mshambuliaji wa Paris St-Germain Kylian Mbappe amekubali kujiunga na Real Madrid msimu huu wa joto.

Nahodha huyo wa Ufaransa, 25, ameiambia PSG kuwa ana nia ya kuondoka klabu hiyo huku kandarasi yake ikikamilika mwezi Juni.

Mbappe bado hajasaini mkataba na Real, lakini dili hiyo inaweza kutangazwa mara baada ya vilabu hivyo kutokutana tena katika Ligi ya Mabingwa msimu huu.

Mshindi huyo wa Kombe la Dunia ndiye mfungaji bora wa PSG akiwa na mabao 244.

Mbappe alitaka mustakabali wake utatuliwe kabla ya Machi, hivyo mnamo Februari 13, kabla ya mazoezi, alikutana na rais wa PSG Nasser Al-Khelaifi na kumwambia kwamba anaondoka na kujiunga na Real.

Baada ya taarifa kuibuka Alhamisi iliyopita kwamba ataondoka, Mbappe aliachwa kwenye kikosi cha kwanza cha mechi ya Jumamosi dhidi ya Nantes, lakini aliingia akitokea benchi na kufunga penalti huku PSG wakiwa mbele kwa pointi 14 kileleni mwa Ligue 1.

Anatazamiwa kusaini mkataba wa miaka mitano na Real, akipata euro 15m (£12.8m) kwa msimu, pamoja na bonasi ya usajili ya euro 150m (£128m) ambayo atalipwa kwa miaka mitano, na atabakia na asilimia fulani ya haki zake za picha.

Meneja wa Real Carlo Ancelotti tayari amefikiria jinsi atakavyomtumia Mbappe katika timu yake, huku kiungo wa kati wa Uingereza Jude Bellingham akicheza nafasi ya kina, Mbrazil Vinicius Jr akicheza upande wa kushoto na Mbappe akicheza kushoto katikati.