• Akijiunga tena na wababe hao wa Italia bila malipo, Pogba alikuwa amekaa kwa misimu sita iliyopita Manchester United, akiwa na wakati mgumu.
Kiungo wa Juventus na Ufaransa, Paul Pogba amefungiwa kujihusisha na soka kwa miaka minne kutokana na makosa ya kutumia dawa za kusisimua misuli.
La Repubblica limeripoti kuwa Pogba na timu yake wamekubali kufungiwa miaka minne kutoka kwa Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Kupambana na Dawa za Kulevya.
Mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United na kiungo wa sasa wa Juventus alipimwa na kukutwa na testosterone iliyopigwa marufuku baada ya mechi dhidi ya Udinese mnamo Agosti 20, 2023.
Pogba anatimiza umri wa miaka 31 mwezi Machi 15, na marufuku hiyo ya muda mrefu inaweza kumaliza maisha yake ya soka.
Mshindi huyo wa Kombe la Dunia la Ufaransa alitumia muda wote wa mchezo wa Udinese kwenye benchi, na kisha akaingia kama mchezaji wa akiba dhidi ya Bologna na Empoli, lakini hajacheza soka tangu kesi hiyo ilipotangazwa hadharani Septemba 11.
La Repubblica inadai mwendesha mashtaka hakuwahi kuamini toleo la upande wa utetezi la ulaji wa testosterone kwa bahati mbaya, ambayo ilikuwa sababu kuu ya mawakili wa Pogba kukataa makubaliano ya rufaa, hatua ambayo ingewezekana angalau kupunguza nusu ya marufuku.
Mnamo Septemba 11, Mahakama ya Kitaifa ya Kupambana na Dawa za Kulevya ilitoa taarifa ikisema: "Tunatangaza kwamba, kwa kukubali ombi lililopendekezwa na Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Kitaifa wa Kupambana na Dawa za Kulevya, tumechukua hatua za tahadhari kumsimamisha mwanariadha huyo:
Paul Labile Pogba ukiukaji wa vifungu 2.1 na 2.2; dutu iliyopatikana: Metaboli ya Testosterone isiyo ya asili (matokeo ya GC/c/IRMS yanaoana na asili ya nje ya metabolites)”.
Akijiunga tena na wababe hao wa Italia bila malipo, Pogba alikuwa amekaa kwa misimu sita iliyopita Manchester United, akiwa na wakati mgumu.
United ilimsajili kiungo huyo kutoka Juve mwaka 2016 kwa rekodi ya dunia ya Pauni 89.3 milioni, na alishinda Ligi ya Europa na Kombe la Ligi katika msimu wake wa kwanza.