Hata namba 5 anaweza shiriki Champions League, hiyo ndio tunapigania sasa – Erik Ten Hag

Baada ya kichapo hicho, Ten Hag sasa anahisi kwamba huenda Man U kumaliza katika nafasi ya 4 ikawa kibarua kigumu na kukiri kwamba wanapambania nafasi ya 5 tu.

Muhtasari

• Ten Hag alisema kwamba hata nafasi ya 5 huenda akapata bahati ya kushiriki ligi ya mabingwa na hilo ndilo lengo lao kwa sasa.

Kocha Erik Ten Hag
Kocha Erik Ten Hag
Image: MUTV

Kocha Erik ten Hag alihisi kuwa kikosi chake cha Manchester United kilifanya vyema kwenye Uwanja wa Etihad na hawakubahatika kurejea Old Trafford wakiwa na angalau pointi moja.

Marcus Rashford aliifungia Reds bao la kuongoza dakika ya nane, akimpita Ederson kutoka umbali wa yadi 25, lakini Phil Foden alifunga bao mbili kwa City, kabla ya Erling Haaland kusuluhisha mambo dakika za majeruhi.

Mholanzi huyo alifurahishwa na jinsi timu yake ilivyotekeleza maagizo yake, akihisi kuwa yamebatilishwa katika 'wakati fulani', haswa baada ya Rashford na Alejandro Garnacho kupewa faulo kufuatia hatua za mwisho kutoka kwa Kyle Walker na Ederson kwa mtiririko huo.

Baada ya kichapo hicho, Ten Hag sasa anahisi kwamba huenda Man U kumaliza katika nafasi ya 4 ikawa kibarua kigumu na kukiri kwamba wanapambania nafasi ya 5 tu.

Ten Hag alisema kwamba hata nafasi ya 5 huenda akapata bahati ya kushiriki ligi ya mabingwa na hilo ndilo lengo lao kwa sasa.

Huu hapa ni muhtasari wa nukuu ambazo Ten Hag alizitoa kwa MUTV, Sky Sports, BBC na vyombo vingine vya habari baada ya filimbi ya mwisho huko Manchester Mashariki…

“Nadhani tunaendelea kweli. Lazima urejeshe pointi kadhaa, halafu lazima ushinde mchezo kama wa leo dhidi ya City. Na kuna michezo zaidi inayokuja. Bado kuna michezo mingi ya kucheza na kila mtu anaweza kushinda kila mtu.”

“Kwa hivyo mambo yanaweza kugeuka haraka. Kwa hivyo lazima tushinde michezo yetu. Nambari tano inaweza kuwa nafasi ya Ligi ya Mabingwa, kwa hivyo, kama ninavyosema, lazima tupiganie.”