logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Nottingham Forest yavunja kimya baada ya Ligi Kuu kuipokonya pointi 4

Klabu ilielezea kusikitishwa kwake na mashtaka na ushahidi uliowasilishwa dhidi yao na ligi kuu ikitaja kuwa hayakutarajiwa.

image
na Samuel Maina

Michezo19 March 2024 - 05:24

Muhtasari


  • •Nottingham Forest ilipata pigo kubwa Jumatatu jioni baada ya kupokonywa pointi nne kutoka kwa jumla ya pointi zao msimu huu.
  • •Klabu ilielezea kusikitishwa kwake na mashtaka na ushahidi uliowasilishwa dhidi yao na ligi kuu ikitaja kuwa hayakutarajiwa.

Siku ya Jumatatu jioni, klabu ya soka ya Nottingham Forest ilipata pigo kubwa baada ya kupokonywa pointi nne kutoka kwa jumla ya pointi zao msimu huu.

Klabu hiyo yenye maskani yake Nottinghamshire ilikabiliwa na adhabu hiyo baada ya tume ya Ligi Kuu kuipata na hatia ya kukiuka kanuni za faida na uendelevu.

Katika taarifa iliyotolewa baada ya adhabu hiyo, klabu hiyo ilieleza kusikitishwa kwake na uamuzi huo ulioirudisha hadi nambari 18 kwenye jedwali la Ligi Kuu ya Uingereza ikiwa na pointi 21 pekee kati ya mechi 29 ilizocheza.

"Nottingham Forest imesikitishwa sana na uamuzi wa Tume ya kuweka adhabu kwa Klabu ya kupokonywa pointi nne, kutumika mara moja," taarifa iliyochapishwa na Nottingham Forest kwenye tovuti yake rasmi ilisomeka.

Ilisomeka zaidi, “Pamoja na kusikitishwa kwetu, tunaishukuru Tume kwa kukubali kushughulikia suala hili kwa haraka. Klabu inaona kuwa ni muhimu kwa uadilifu wa ligi kusuluhisha mashtaka katika msimu ambao yatatolewa."

Klabu hiyo pia ilielezea kusikitishwa kwake na mashtaka na ushahidi uliowasilishwa dhidi yao na ligi kuu ikitaja kuwa hayakutarajiwa.

"Baada ya miezi kadhaa ya mazungumzo na Ligi Kuu, na ushirikiano wa kipekee wakati wote, hii haikutarajiwa na imeharibu imani na imani tuliyokuwa nayo katika Ligi Kuu," ilisema.

Klabu hiyo sasa imedokeza kuhusu kukata rufaa kwa uamuzi huo ili kuona kama adhabu ya kupokonywa kwa pointi nne itabatilishwa.

Nottingham Forest ni klabu ya pili kukatwa pointi msimu huu baada ya Everton kupokwa pointi 10 mapema msimu huu kwa kukiuka kanuni za faida za Ligi ya Premia.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved