Real yalalamikia hatua ya refa kupuuza unyanyasaji wa kibaguzi dhidi ya Vinicius Jr

Klabu hiyo inasema "matusi na kelele za kuudhi" "hazikujumuishwa kwa makusudi" na Juan Martinez Munuera.

Muhtasari

•Real imewasilisha malalamiko dhidi ya mwamuzi aliyesimamia mechi ya Jumamosi dhidi ya Osasuna kwa kupuuza unyanyasaji wa kibaguzi.

Vinicius Junior
Image: BBC

Real Madrid imewasilisha malalamiko dhidi ya mwamuzi aliyesimamia mechi ya Jumamosi huko Osasuna kwa kupuuza unyanyasaji wa kibaguzi dhidi ya mshambuliaji Vinicius Jr kutoka kwa ripoti yake ya mechi.

Klabu hiyo inasema "matusi na kelele za kuudhi" "hazikujumuishwa kwa makusudi" na Juan Martinez Munuera.

Vinicius amekumbana na ubaguzi wa rangi mara kadhaa nchini Uhispania katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

Real watakai "hatua madhubuti zichukuliwe" ili "kutokomeza" unyanyasaji huo.

Kamati ya ufundi ya waamuzi wa Shirikisho la Soka la Uhispania imetafutwa ili kutoa maoni yake.

Real ilisema: "Mwamuzi kwa hiari na kwa makusudi aliacha matusi na kelele za kuudhi zilizoelekezwa mara kwa mara kwa mchezaji wetu Vinicius Jr, licha ya haya kuonyeshwa kwa msisitizo na wachezaji wetu wakati yalipokuwa yakifanyika.

"Real Madrid kwa mara nyingine inalaani mashambulizi haya makali ya ubaguzi wa rangi, ubaguzi na chuki, na inataka hatua zinazofaa zichukuliwe, mara moja na kwa wote, kutokomeza vurugu ambazo mchezaji wetu Vinicius Junior amekuwa akikumbana nayo."