Madowo afichua mazungumzo mazuri aliyoshiriki na Olunga kabla ya kufunga hat-trick dhidi ya Zimbabwe

Olunga mbaye pia alikuwa akisherehekea siku yake ya kuzaliwa alifunga mabao matatu na kuipa timu ya taifa ushindi wa 3-1.

Muhtasari

•Baada ya mchuano huo, Madowo alimpongeza mshambuliaji huyo kwa kiwango kizuri na kumtakia heri ya siku ya kuzaliwa.

•Olunga alionyesha mchezo mzuri, akifunga hat-trick katika mechi hiyo na kuipa Kenya ushindi mkubwa dhidi ya Zimbabwe.

 

Larry Madowo amefichua mazungumzo mazuri alishiriki na Olunga
Image: HISANI

Mwanahabari wa kimataifa wa Kenya Larry Madowo amefichua mazungumzo mazuri ambayo alikuwa nayo na mshambuliaji Michael Olunga siku ya Jumanne, kabla ya mechi kati ya Harambee Stars na Zimbabwe.

Nahodha huyo wa Harambee Star ambaye pia alikuwa akisherehekea siku yake ya kuzaliwa mnnamo siku ya mechi hiyo alifunga mabao matatu na kuipa timu ya taifa ya Kenya ushindi wa 3-1 dhidi ya The Warriors wa Zimbabwe.

Kabla ya mechi hiyo, mwanahabari Larry Madowo ambaye kwa sasa anafanya kazi CNN alikuwa amemtakia kila la heri mshambuliaji huyo wa Al-Duhail SC katika mchuano huo wa fainali.

“Kila la heri dhidi ya Zimbabwe! Wachape kama Malawi!” Madowo alimwandikia Olunga.

Katika majibu yake, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 alionekana kukubaliana na Madowo na kudokeza kuhusu mchezo mzuri.

“Kabisa kaka yangu,” alijibu.

Kwa kweli, kama alivyosema, nahodha huyo wa Harambee stars alionyesha mchezo mzuri, akifunga hat-trick katika mechi hiyo na kuipa Kenya ushindi mkubwa dhidi ya Zimbabwe.

Baada ya mchuano huo, Madowo alimpongeza mshambuliaji huyo kwa kiwango kizuri na kumtakia heri ya siku ya kuzaliwa.

“Mazungumzo yangu na nahodha Michael Olunga hapo awali. Form ni kusema na kutenda! Heri ya kuzaliwa, kaka,” mwandishi huyo wa habari wa CNN aliandika huku akifichua mazungumzo yao.

Image: FACEBOOK// LARRY MADOWO

Harambee Stars mnamo Jumanne ilijiondoa katika mchujo na kunyakua taji la Mashindano ya Mataifa Nne baada ya kulaza Zimbabwe 3-1 kwenye Uwanja wa Bingu mjini Lilongwe, Malawi, kwa bao la hat-trick la Michael Olunga.

Vijana wa nyumbani walianza kwa mkondo mbaya baada ya makosa ya Joseph Okumu katika hatua za mapema za mchezo kuwapa wapinzani wao bao la kwanza na bao lao la pekee katika dakika ya tatu.

Lakini zikiwa zimesalia dakika mbili tu kabla ya mapumziko, Olunga mwenye hirimu alisawazisha mambo baada ya kutumia vyema pasi ya Ayub Timbe iliyowekwa kwenye eneo la hatari na kumshinda mlinzi huyo wa Zimbabwe.

Olunga, ambaye anachezea Qatar Al-Duhail, alifunga tena dakika ya 62 aliposonga mbele na kufanya mambo kuwa 2-1.

Zikiwa zimesalia dakika nne tu kabla ya kipenga cha mwisho kumalizika, mshambuliaji huyo mwenye mvuto alifunga hatima ya mpinzani wao baada ya kushambulia mpira wa Timbe na kufanya mambo kuwa 3-1 na kupata ushindi huo muhimu kwa Stars.