Erik ten Hag: Kocha wa Man United asema 'hajali' kuhusu uvumi wa kazi yake

Kundi la Sir Jim Ratcliffe la Ineos linaripotiwa kufikiria kufanya marekebisho ya ukufunzi msimu huu wa joto.

Muhtasari

•Kocha wa England Gareth Southgate amehusishwa lakini akasema hiyo ni "kufuru kabisa" kwani ni kazi ya Ten Hag.

Erik ten Hag
Erik ten Hag
Image: HISANI

Mkufunzi wa Manchester United Erik ten Hag anasema hajali kuhusu uvumi unaohusu kibarua chake.

Kundi la Sir Jim Ratcliffe la Ineos linaripotiwa kufikiria kufanya marekebisho ya ukufunzi msimu huu wa joto.

Kocha wa England Gareth Southgate amehusishwa lakini akasema hiyo ni "kufuru kabisa" kwani ni kazi ya Ten Hag.

"Unajua huko Man United kutakuwa na kelele kila wakati, uvumi karibu na klabu, meneja, wachezaji," Ten Hag alisema.

"Tunaangazia mchakato, tunaangazia timu kucheza vizuri zaidi, kuboresha njia ya uchezaji, kwa hivyo sijali [hilo]."

Meneja wa Wolves Gary O'Neil pia ameripotiwa kutazamwa na United tangu Ineos achukue shughuli za soka, lakini amekanusha kuhusishwa na Old Trafford.