Kocha mkongwe wa Arsenal adai Martin Ødegaard alimkumbusha Fabregas alipomkuta 2014

"Namkumbuka sana. Tulipigana kama wazimu ili kumpata, lakini mwishowe, alichagua kwenda Real Madrid,” Wenger alimwambia Ljungberg.

Muhtasari

• Hata hivyo, inafaa ikumbukwe kwamba Odegaard mwishowe alipeanwa kwa mkopo kutoka Real Madrid kwenda Arsenal kabla ya kusainiwa kabisa msimu uliofuata.

• Odegaard sasa ni mmoja wa viungo wabunifu wa Premier League na alitia saini mkataba mpya mwaka jana wa kusalia Arsenal hadi angalau msimu wa joto wa 2027.

Nahodha wa Arsenal, Martin Odegaard
Nahodha wa Arsenal, Martin Odegaard
Image: HISANI

Kocha mkongwe wa Arsenal, Arsene Wenger amekiri mara ya kwanza alipokutana na nahodha wa sasa wa The Gunners, Martin Odegaard, aliona chembechembe za aliyekuwa mchezaji wa klabu hiyo, Cesc Fabregas.

Katika mazungumzo na lejendari wa The Gunners, Freddie Ljungberg, Wenger alisema kwamba Odegaard mara ya kwanza kukutana naye ilikuwa mwaka wa 2014 na licha ya kumfanyia hadi vipimo vya afya tayari kumsaidi, mchezaji huyo kipindi hicho alichagua kuitumikia Real Madrid na kuikataa Arsenal.

Hata hivyo, inafaa ikumbukwe kwamba Odegaard mwishowe alipeanwa kwa mkopo kutoka Real Madrid kwenda Arsenal kabla ya kusainiwa kabisa msimu uliofuata.

“Namkumbuka sana. Tulipigana kama wazimu ili kumpata. Nilimpeleka kwenye kikao cha mazoezi na nakumbuka Steve Morrow alimleta kwenye mazoezi na baba yake.”

"Alinikumbusha Fabregas - maono mazuri, ubora mzuri wa kiufundi, rahisi na wachezaji wa kulipwa katika kikosi cha kwanza. Unaweza kuona kitu cha pekee pale lakini mwishowe, alichagua kwenda Real Madrid,” Wenger alimwambia Ljungberg.

Odegaard sasa ni mmoja wa viungo wabunifu wa Premier League na alitia saini mkataba mpya mwaka jana wa kusalia Arsenal hadi angalau msimu wa joto wa 2027.

Raia huyo wa Norway alisema wakati huo: "Kusaini mkataba mpya ulikuwa uamuzi rahisi kwangu kwa sababu nyingi.”

"Hasa kile tunachofanya hivi sasa kama klabu ni maalum, na ninataka kuwa sehemu ya hiyo. Nimefurahiya sana kitakachokuja hapa. Nimepata mahali ambapo ninaweza kutulia na kupiga simu nyumbani kwangu.”

 

"Hadithi yangu ni tofauti labda, nilipozunguka vilabu tofauti tangu nikiwa na umri wa miaka 16. Nikiwa Arsenal, tangu siku ya kwanza, nimejisikia vizuri na hii ni nyumbani kwangu sasa.

"Nataka tu kusema asante kwa kila mtu anayefanya kazi kwenye kilabu na bila shaka, wafuasi wetu wazuri. Nitaendelea kutoa kila kitu ili kuleta mafanikio kwa klabu hii katika miaka ijayo.”