Beki wa Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini afariki baada ya kutekwa nyara na kuuawa

Ripoti hiyo ilisema beki huyo wa kati alitekwa nyara jijini Johannesburg usiku wa kuamkia Aprili 4 kabla ya kuuawa saa chache baadae.

Muhtasari

• Beki huyo wa kati aliyesajiliwa na Kaizer mwezi October 2023 amefariki akiwa na umri wa miaka 24 baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana.

• Kaizer Chiefs walisema kwamba tayari kesi hiyo inashughulikiwa na polisi wa kupambana na uhalifu.

Luke Fleurs, beki aliyeuawa.
Luke Fleurs, beki aliyeuawa.
Image: Instagram//KaizerChiefsfc

Klabu ya mpira wa miguu nchini Afrika Kusini, Kaizer Chiefs FC imetangaza kifo cha mchezaji wao ambaye ilidai aliuawa na watekaji nyara jijini Johannesburg.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo kwenye ukurasa wao rasmi wa Instagram, Kaizer Chiefs walisema beki wao kwa jina Luke Fleurs alitekwa nyara usiku wa kuamkia Aprili 4 jijini Johannesburg kabla ya kuuawa.

“Ni kwa huzuni kubwa kwamba tunatangaza kwamba mchezaji wa Kaizer Chiefs, Luke Fleurs alipoteza maisha yake jana usiku wakati wa tukio la utekaji nyara huko Johannesburg. Mawazo na sala zetu ziko pamoja na familia yake na marafiki katika wakati huu mgumu,” sehemu ya ripoti hiyo ilisoma ikiambatanishwa na picha na beki huyo.

Beki huyo wa kati aliyesajiliwa na Kaizer mwezi October 2023 amefariki akiwa na umri wa miaka 24 baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana.

Kaizer Chiefs walisema kwamba tayari kesi hiyo inashughulikiwa na polisi wa kupambana na uhalifu.

“SAPS inashughulikia suala hilo na maelezo zaidi yatawasilishwa kwa wakati ufaao. Roho yake mpendwa ipumzike kwa Amani.”