Ronaldo sasa amefikisha kadi nyekundu mara nne zaidi ya Messi, "GOAT kwa kila kitu, eeh!"

Ronaldo sasa ana jumla ya kadi 12 nyekundu dhidi ya 3 za Messi. Kufukuzwa kwake mara nane kati ya 12 kulitokana na kadi nyekundu ya moja kwa moja, ikiwa ni pamoja na kushindwa kwa Jumatatu dhidi ya Al Hilal.

Muhtasari

• Messi, kwa upande mwingine, amepata kadi nyekundu tatu katika maisha yake ya soka hadi sasa. Zote za kufukuzwa kwake zilikuwa nyekundu moja kwa moja.

• Kadi nne kati ya 12 nyekundu za Ronaldo zilipatikana wakati akiwa na Manchester United, zote zilitokea kwenye mechi za Ligi Kuu ya Uingereza

Messi na Ronaldo.
Messi na Ronaldo.
Image: Facebook

Nguli wa mchezo wa soka kutoka Ureno, Cristiano Ronaldo sasa amefikisha idadi ya kadi nyekundu, mara nne Zaidi ya mshindani wake ambaye wanalinganishwa katika kila kitu, Muargetina Lionel Messi.

Kadi nyekundu dhidi ya Al Hilal usiku wa jana kwenye kombe la Saudi Super Cup ilifikisha idadi ya kadi nyekundu 12 ambazo mkongwe huyo wa miaka 39 amewahi onyeshwa katika taaluma yake ya kandanda ya Zaidi ya miaka 20.

Kufukuzwa kwake mara nane kati ya 12 kulitokana na kadi nyekundu ya moja kwa moja, ikiwa ni pamoja na kushindwa kwa Jumatatu dhidi ya Al Hilal.

Messi, kwa upande mwingine, amepata kadi nyekundu tatu katika maisha yake ya soka hadi sasa. Zote za kufukuzwa kwake zilikuwa nyekundu moja kwa moja.

Kadi nne kati ya 12 nyekundu za Ronaldo zilipatikana wakati akiwa na Manchester United, zote zilitokea kwenye mechi za Ligi Kuu ya Uingereza.

Kadi yake nyekundu ya kwanza akiwa mtaalamu ilitokea kwenye mchezo dhidi ya Aston Villa mnamo Mei 15, 2004, huku nyota huyo wa Ureno akipewa maagizo yake dakika ya 85.

Kufukuzwa kwake mara mbili akiwa na United kulitokea kwenye mechi ya Manchester derby. Alionyeshwa kadi nyekundu katika ushindi wa 3-1 wa City dhidi ya United Januari 14, 2006, baada ya kumchezea vibaya Andy Cole.