Fahamu sababu ya mlinzi wa kibinafsi wa Messi alipigwa marufuku kuingia uwanjani

Chueko ni mwanajeshi wa zamani wa Jeshi la Marekani na ametumikia Iraq na Afghanistan kama jeshi la wanamaji la Navy Seal

Muhtasari

• Chueko pia anasemekana kuongoza timu ya watu 50, wanaofanya kazi usiku kucha kuwaweka salama Messi na wapendwa wake huko Miami.

Messi na mlinzi wake
Messi na mlinzi wake
Image: Maktaba

Mlinzi wa Lionel Messi Yassine Chueko alipigwa marufuku kuingia uwanjani Monterrey siku ya Jumatano kwa ajili ya mechi ya robo fainali ya Kombe la Mabingwa wa CONCACAF ya Inter Miami kufuatia mzozo mkali.

Inter Miami wanaelekea kwenye mchezo wa Jumatano dhidi ya Mexico kwa mabao 2-1 kufuatia kushindwa kwenye ardhi ya nyumbani - mchezo ambao Messi hakushiriki lakini hilo halikumzuia Muargentina huyo aliyeshinda Kombe la Dunia kujihusisha na hali mbaya.

Messi alizozana vikali na kocha msaidizi wa Monterrey, Nico Sanchez baada ya Inter Miami kuonyesha kutofurahishwa na wasimamizi wa mechi hiyo, ambao waliwaonyesha timu hiyo ya MLS kadi sita za njano na nyekundu.

Sanchez alimtaja Messi kama "kibeti aliyemilikiwa" ambaye ana "uso wa shetani" katika sauti iliyovuja baada ya kudaiwa "kuweka ngumi" karibu na uso wa kocha huyo.

Sanchez tangu wakati huo ameomba radhi kwa kauli yake iliyomlenga Messi na kocha mkuu wa Inter Miami, Tata Martino, lakini hakupunguza mvutano kuelekea mechi ya marudiano ya Jumatano, ambayo mshindi huyo mara nane wa Ballon d'Or atacheza.

Kwa mujibu wa Canal 6, Inter Miami itaadhibiwa kifedha na CONCACAF kwa matukio hayo machafu, huku Messi pia alifahamishwa kuwa mlinzi wake Chueko atapigwa marufuku kuingia uwanjani.

Chueko ataruhusiwa tu katika vyumba vya kubadilishia nguo na eneo la mchanganyiko.

Chueko ni mwanajeshi wa zamani wa Jeshi la Marekani na ametumikia Iraq na Afghanistan kama jeshi la wanamaji la Navy Seal, kulingana na La Nacion, na ana mamia ya maelfu ya wafuasi wa Instagram. Inaripotiwa kuwa Chueko alipendekezwa na mmiliki mwenza wa Inter Miami David Beckham.

Chueko pia anasemekana kuongoza timu ya watu 50, wanaofanya kazi usiku kucha kuwaweka salama Messi na wapendwa wake huko Miami.

Mara nyingi ameonekana akishika doria wakati wa michezo ili kuwanasa mashabiki wanaokimbia uwanjani kujaribu kukutana na sanamu wao wa soka.