Mechi ya Udinese dhidi ya Roma ililazimika kusitishwa baada ya beki kuzirai uwanjani

Beki huyo wa Roma mwenye umri wa miaka 24 alitoka nje ya uwanja kwa machela kunako dakika 72 kwenye Uwanja wa Bluenergy.

Muhtasari

• “Mchezaji huyo ana fahamu na amepelekwa hospitali kwa uchunguzi zaidi. Forza Evan, sote tuko pamoja nawe!”

• Udinese walitweet kwa urahisi: "Tuko pamoja nawe, Ndicka."

Evan Ndicka wakati wa pambano dhidi ya Udinese.
Evan Ndicka wakati wa pambano dhidi ya Udinese.
Image: X//AS Roma

Pambano la Jumapili la Serie A kati ya Udinese na Roma lilisitishwa baada ya mchezaji wa kimataifa wa Ivory Coast Evan Ndicka kuzimia uwanjani.

Beki huyo wa Roma mwenye umri wa miaka 24 alitoka nje ya uwanja kwa machela kunako dakika 72 kwenye Uwanja wa Bluenergy.

Klabu yake baadaye ilithibitisha kuwa mchezaji huyo wa zamani wa Auxerre na Eintracht Frankfurt alikuwa na fahamu na alikuwa amepelekwa hospitali kuchunguzwa.

Taarifa kwenye akaunti ya X rasmi ya Roma - iliyokuwa akaunti ya Twitter - ilisomeka: "Kufuatia dharura ya matibabu ya uwanjani iliyomhusisha Evan Ndicka, mechi kati ya Udinese na Roma imesimamishwa.”

“Mchezaji huyo ana fahamu na amepelekwa hospitali kwa uchunguzi zaidi. Forza Evan, sote tuko pamoja nawe!”

Udinese walitweet kwa urahisi: "Tuko pamoja nawe, Ndicka."

Roberto Pereyra alikuwa ameipatia timu ya nyumbani bao la kuongoza kabla ya mapumziko, lakini Romelu Lukaku akafanya matokeo kuwa 1-1 zikiwa zimepita dakika 64.

Taarifa hiyo iliongeza: "Ataendelea kuwa chini ya uangalizi kwa ajili ya vipimo hospitalini."

Ndicka alijiunga na Roma kwa uhamisho wa bure kutoka Eintracht Frankfurt mwaka 2023 na amecheza mechi 19 katika klabu hiyo ya Italia.

Mechi iliyosalia sasa imepangwa kuchezwa baadaye.