Rainford Kalaba: Nahodha wa zamani wa Zambia yuko katika hali 'mbaya lakini dhabiti' baada ya ajali mbaya

Faz inasema Kalaba, ambaye yuko hospitalini, alipata "majeraha ya ndani".

Muhtasari
  • Nyota huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 37 alikuwa abiria katika gari aina ya Mercedes Benz ilipogongana na lori lililokuwa likija katika mji wa Kafue kusini-mashariki mwa Zambia.
Rainford Kalaba
Image: KWA HISANI

Nahodha wa zamani wa Zambia, Rainford Kalaba yuko katika hali "mbaya lakini dhabiti" kufuatia ajali mbaya ya barabarani siku ya Jumamosi, kulingana na chama cha soka cha nchi hiyo (Faz).

Nyota huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 37 alikuwa abiria katika gari aina ya Mercedes Benz ilipogongana na lori lililokuwa likija katika mji wa Kafue kusini-mashariki mwa Zambia.

Dereva wa kike wa gari alilokuwa akisafiria Kalaba aliaga dunia

Faz inasema Kalaba, ambaye yuko hospitalini, alipata "majeraha ya ndani".

Ripoti ya polisi iliyotolewa baada ya ajali hiyo ilisema uchunguzi wa awali unaonyesha ajali hiyo ilitokana na hatua ya gari hilo la mercedes "kulipita vibaya" lori hilo.

Habari kuhusu Kalaba zinafuatiliwa kwa karibu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambako mshambuliaji huyo aliichezea TP Mazembe kati ya 2011 na 2023.

Kulikuwa na mkanganyiko juu ya hali ya Kalaba mara baada ya ajali hiyo wakati Mazembe ilipotuma taarifa kwenye mitandao ya kijamii ambazo klabu hiyo imezitolea ufafanuzi.