Thiago Silva amethibitisha kuondoka kwa Chelsea katika ujumbe wa hisia kwa mashabiki

Amecheza mechi 151 kwa jumla akiwa na Chelsea na anasubiri matokeo ya uchunguzi wa jeraha la paja, huku kukiwa na hofu kuwa amecheza mechi yake ya mwisho kwa The Blues.

Muhtasari

• "Tayari ni ngumu kusema kwaheri katika hali ya kawaida, lakini kunapokuwa na upendo wa pande zote, ni ngumu zaidi. Lakini mara moja Bluu, daima ni Bluu.

Thaigo Silva
Thaigo Silva
Image: Facebook

Thiago Silva amethibitisha kwamba ataondoka Chelsea mkataba wake utakapomalizika mwishoni mwa msimu huu.

Beki huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 39 alitangaza kuondoka Jumatatu asubuhi katika ujumbe wa hisia kwa mashabiki uliotumwa kupitia tovuti rasmi ya Chelsea na mitandao ya kijamii.

Silva alijiunga na Chelsea kwa uhamisho wa bure kutoka Paris Saint-Germain mwaka 2020 na alikuwa sehemu ya kikosi kilichoshinda Ligi ya Mabingwa mwaka 2021.

Amecheza mechi 151 kwa jumla akiwa na Chelsea na anasubiri matokeo ya uchunguzi wa jeraha la paja, huku kukiwa na hofu kuwa amecheza mechi yake ya mwisho kwa The Blues.

Silva alitoka katika jeraha katika mchezo wa Jumamosi wa sare ya 2-2 dhidi ya Aston Villa na anafanyiwa vipimo ambavyo vitaamua kama anaweza kucheza tena msimu huu.

Silva alisema katika ujumbe kwa mashabiki: “Chelsea ina maana kubwa kwangu. Nilikuja hapa kwa nia ya kukaa mwaka mmoja tu na ikaishia miaka minne. Sio kwangu tu bali kwa familia yangu pia.

"Wanangu wanachezea Chelsea kwa hivyo ni fahari kubwa kuwa sehemu ya familia ya Chelsea - kwa sababu wanangu wapo hapa. Natumai wanaweza kuendeleza maisha yao hapa katika klabu hii ya ushindi ambayo wachezaji wengi wanatamani kuwa sehemu yake.

"Nadhani katika kila kitu nilichofanya hapa kwa miaka minne, kila wakati nilitoa kila kitu. Lakini, kwa bahati mbaya, kila kitu kina mwanzo, katikati na mwisho. Hiyo haimaanishi kuwa huu ni mwisho wa uhakika. Natumai kuacha mlango wazi ili katika siku za usoni niweze kurudi, ingawa katika jukumu lingine hapa.

"Lakini ... ni upendo usioelezeka. Naweza kusema tu asante.

"Ni wazi, nilipoanza hapa, ilikuwa wakati wa janga kwa hivyo hakukuwa na mashabiki kwenye uwanja. Lakini kupitia mitandao ya kijamii ikawa ni kitu cha kipekee sana kwangu ndipo mashabiki walipoanza kurejea uwanjani na maisha yakawa yanarudi kawaida nilianza kuhisi mapenzi na heshima kubwa kwa stori yangu na kwa kuanzia kwangu hapa.

"Tayari ni ngumu kusema kwaheri katika hali ya kawaida, lakini kunapokuwa na upendo wa pande zote, ni ngumu zaidi. Lakini mara moja Bluu, daima ni Bluu.