Bundesliga yapata nafasi ya ziada katika ligi ya mabingwa 2024/25

Timu za Bundesliga zinapata nafasi ya ziada kwa 2024/25.

Muhtasari

•Timu nne zinazowania kubeba ubigwa wa Ulaya.

•Timu za Bundesliga zinapata nafasi ya ziada kwa 2024/25.

Matokeo ya hatua ya kwanza
Image: Hisani

Nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya  hatua ya kwanza ilianza kwa  kufurahisha na mchezo wa kusisimua. Kwa siku mbili zilizopita, ulimwengu wa soka ulishuhudia mapambano kati ya timu nne zinazowania kubeba ubigwa wa Ulaya.

Nusu fainali ya kwanza ilishuhudia makabiliano kati ya mabingwa mara kwa mara Bayern Munich wa Ujerumani na  Real Madrid kutoka Uhispania.

Timu zote mbili zilikua na mchezo mzuri. Bayern Munich, wakiongozwa na hamu yao ya kulinda ubingwa wao, walituma mashambulizi yasio na mwisho, wakijaribu kuzimi azimio ya Real Madrid kutamba kwenye pambano hilo.

Pambano hilo iliisha sare ya mabao mawili, wiki ijawayo Real Madrid watakuwa wenyeji wa Bayern Munich katika hatua ya pili ambapo kila timu itakua na hamu ya kuingia fainali.

Pambano lingine ilishuhudia Borussia Dortmund kutoka Ujerumani ilikutana na Paris Saint-Germain ya Ufaransa.

 Timu zote mbili zilionyesha ustadi wao wa kushambulia na azimio lao la kufika fainali. Borussia Dortmund, walitumia uwanja wao wa  nyumbani na kuonyesha mchezo mzuri na baada ya kipenga cha mwisho walikua washindi.

Pambano hizo zitarejelewa kwa mara ya  pili wiki ijayo na kila timu itakua inawania kufika fainali na kubeba taji hilo la Mabigwa Ulaya.

Ushindi wa Borussia Dortmund dhidi ya PSG usiku wa kuamkia leo umefanya  Ligi ya Italia kuwakilishwa na  timu tano katika  michezo wa Mabingwa Ulaya msimu ujao na ina maana kwamba ni timu nne tu bora za Ligi Kuu ya Uingereza zitafuzu.