Leicester, Ipswich warejea EPL huku Leeds, Southampton, West Brom na Norwich wakisubiri kujua hatima yao

Ipswich Town wamehangaika kwa miaka 22 kurejea ligi kuu na haijakuwa safari rahisi.

Muhtasari

•Ushindi wa Leicester City pia uliwarudisha kwenye Ligi Kuu ya Uingereza, mwaka mmoja tu baada ya kushushwa daraja.

•Leeds, Southampton, West Brom ana Norwich itabidi wakabiliane ili kujua nani atapandishwa daraja.

wamerejea kwenye EPL
Leicester City na Ipswich Town wamerejea kwenye EPL

Ligi ya daraja la pili ya soka nchini Uingereza, Championship, ilimalizika siku ya Jumamosi huku Leicester City wakishinda kombe hilo  baada ya kuibuka nambari moja kwa pointi 97.

Ushindi wa Leicester City pia uliwarudisha kwenye Ligi Kuu ya Uingereza, mwaka mmoja tu baada ya kushushwa daraja hadi Championship.

Klabu ya Ipswich Town ilimaliza nambari mbili kwenye ligi ya Championship kwa pointi 96 na pia ilipata kupanda daraja moja kwa moja hadi ligi kuu baada ya takriban miongo miwili nje ya ligi kuu.

Klabu hiyo ambayo ilipandishwa daraja hadi Ubingwa kutoka League One msimu uliopita ilishiriki ligi kuu mara ya mwisho mwaka wa 2002 iliposhuka daraja.

Kwa miaka 22 wamehangaika kurejea ligi kuu na haijakuwa safari rahisi.

Leeds, Southampton, West Brom ana Norwich walimaliza nafasi ya tatu, nne, tano na sita mtawalia na sasa itabidi wakabiliane ili kujua nani atapandishwa daraja.

Kwa upande mwingine; Birmingham, Huddersfield na Rotherham walishuka daraja hadi League One  baada ya kumaliza nafasi ya 22, 23, na 24 mfululizo.

Wakati huo huo, Sheffield United wanaoshiriki EPL tayari wamerudishwa tena kwenye Championship baada ya kupandishwa daraja msimu uliopita.

Luton Town, Burnley na Nottingham bado wanapambana kubaini ni nani atafanikiwa kusalia kwenye ligi kuu baada ya mechi mbili zilizosalia.