Fahamu kwa nini refa wa mechi ya Crystal Palace dhidi ya Man United alivaa kamera

Video hiyo itatumika katika programu inayotoa maarifa kuhusu usimamizi wa Ligi Kuu

Muhtasari

•Jarred Gillett alitumia kifaa kilichopachikwa kichwa kiitwacho 'RefCam', ingawa picha hazitaonyeshwa moja kwa moja.

Image: BBC

Mwamuzi alivaa kamera ya video kwa mara ya kwanza katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza wakati wa mechi ya Jumatatu kati ya Crystal Palace dhidi ya Manchester United.

Jarred Gillett alitumia kifaa kilichopachikwa kichwa kiitwacho 'RefCam', ingawa picha hazikuonyeshwa moja kwa moja.

Video hiyo itatumika katika programu inayotoa maarifa kuhusu usimamizi wa Ligi Kuu. Mnamo Februari, mwamuzi wa Bundesliga Daniel Schlager alivaa kamera na kipaza sauti wakati wa sare ya 2-2 kati ya Eintracht Frankfurt na Wolfsburg.

Video hiyo pia ilitumika kwa programu inayoitwa 'Referees Mic'd up - Bundesliga'.

Mwaka jana, mwamuzi wa Premier League Rob Jones alivaa kamera kwa ajili ya mechi ya 2023 Summer Series kati ya Chelsea na Brighton mjini Philadelphia.

Utumiaji wa kamera za mwili pia ulijaribiwa na Chama cha Soka katika soka la watu wazima mwaka jana katika juhudi za kupunguza unyanyasaji wa maafisa wa ngazi hiyo.