“Siwezi kuolewa na wewe kwa sababu una pesa nyingi sana” – Jorginho aambiwa na mpenziwe

Kwa mujibu wa takwimu za Capology, Jorginho ndiye mchezaji wa 12 anayelipwa zaidi Arsenal, akipokea mshahara wa pauni 110,000 kwa wiki, sawa na Ksh 18.4M kwa wiki.

Muhtasari

• Mchezaji huyo wa kimataifa wa Italia alisaini Gunners Januari 2023, kwa ada iliyoripotiwa ya pauni milioni 12, akisaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu na chaguo la mwaka zaidi.

Jorginho na mpenziwe Harding
Jorginho na mpenziwe Harding
Image: Hisani

Kuelekea siku yao kubwa ya harusi, Catherine Harding, mpenzi wa mchezaji wa Arsenal na Italia, Jorginho ameshangaza wengi baada ya kufanya mzaha wakati wa mazungumzo yao kwenye gari, akisema kwamba anatathmini kughairi kuolewa na mchezaji huyo.

Mchumba huyo wa Jorginho wakiwa ndani ya gari katika video ambayo kwa sasa ameifuta kutoka kwenye ukurasa wake wa Instagram, alisikika akisema kwa mzaha kwamba hatarajii kufunga ndoa na Jorginho, akisema kwamba mchezaji huyo ana pesa na utajiri mkubwa sana, jambo ambalo linamtia tumbojoto kukubali ndoa naye.

Jorginho alikuwa akiendesha gari, huku wenzi hao wakiwa wameketi kwenye gari lao, huku mwanamitindo huyo akiwarekodi wakiwa na mazungumzo ya kuchekesha.

Klipu hiyo ilionyesha Harding akimwambia mchumba wake kwamba ‘hafikirii wanaweza kuwa pamoja’, kabla ya mwanasoka huyo kushtuka kuuliza kujua kwa nini.

Kiungo huyo wa kati wa Kiitaliano mwenye umri wa miaka 32 alikisia vibaya, kabla ya mwimbaji na mwanamitindo hatimaye kufichua sababu, kama alivyosema:

"Umepata pesa nyingi sana ... [wewe ni] tajiri sana," kabla ya wanandoa waliofunga ndoa hivi karibuni kushiriki kicheko mara moja baadaye.

Kwa mujibu wa takwimu za Capology, Jorginho ndiye mchezaji wa 12 anayelipwa zaidi Arsenal, akipokea mshahara wa pauni 110,000 kwa wiki, sawa na Ksh 18.4M kwa wiki.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Italia alisaini Gunners Januari 2023, kwa ada iliyoripotiwa ya pauni milioni 12, akisaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu na chaguo la mwaka zaidi.

Jorginho alijiunga na klabu hiyo ya Kaskazini mwa London baada ya misimu minne akiwa Chelsea, ambayo alishinda nayo Ligi ya Mabingwa na Ligi ya Europa.

Kulingana na ripoti kadhaa, Jorginho na Catherine Harding wamekuwa wakichumbiana tangu 2020.

Nyota huyo wa zamani wa Chelsea aliachana na mkewe Natalia kabla ya kutoka kimapenzi na Catherine Harding.