Ten Hag aahidi kushinda fainali ya FA

Ten Hag aahidi mashabiki wa Manchester kujitayarisha kupokea kombe la FA nyumbani

Muhtasari

• Ten Hag awahakikishia mashabiki wa United ushindi wa kombe la FA.

• Fainali ya kombe la FA  kuchezwa Jumamosi 25, Mei 2024 ugani Wembley.


Eric Ten Hag Kocha wa Manchester United Picha; Hisani
Eric Ten Hag Kocha wa Manchester United Picha; Hisani

Kocha mkuu wa Manchester United ,Eric Ten Hag ana imani kubwa timu yake itashinda kombe la FA . Ten Hag alisema haya baada ya ushindi wa nyumbani wa 3-2 dhidi ya Newcastle usiku wa Jumatano ,kwenye pambano la ligi kuu ya Uingereza.Kobbie Mainoo, Amad Diallo na Rasmus hojlund walicheka na wavu kila mmoja .

Kwenye mazungumzo na wanahabari baada ya mechi , Ten Hag aliwamiminia sifa mashabiki huku akiwaahidi wachezaji wake watafanya juu chini ili kuleta kombe la FA nyumbani .

'Ninawaahidi kwamba wachezaji watafanya kila kitu ili kuleta kombe hapa Old Trafford...' alisema Ten Hag

Manchester United itachuana na Manchester City kwenye fainali ya kombe la FA Jumamosi 25, Mei 2024 ugani Wembley. Manchester City ambao ni mabingwa watetezi wameshinda kombe hilo mara saba na pia watakuwa kwenye mishemishe za kusaka ubingwa huo kwa mara nyingine.

Aidha ni fursa nyingine kwa Ten Hag kujiliwaza baada ya kuwa na fomu mbaya ligini.Ikiwa watanyakuwa kombe hilo , basi watakuwa wamejihakikishia nafasi kwenye mashindano ya bara Ulaya, msimu ujao.

Je , Ten Hag ataweka furaha kwa nyuso za wana Manchester?