Arsenal wabembeleza West Ham kutendea haki kwa kuipiga Man City, “Do it for London please!”

Baadhi ya mashabiki wa Arsenal walifurika katika kurasa za mitandaoni za West Ham wakiahidi ofa za 'ajabu' kwao iwapo watasaidia ndugu yao kutoka London [Arsenal] kushinda ligi kwa kuipiga breki Man City.

Muhtasari

• Kumbuka kuwa Arsenal vs Everton, na Man City vs West Ham United michezo itaanza saa 4 asubuhi. Jumapili, Mei 19, wakati huo huo.

ARSENAL
ARSENAL
Image: FACEBOOK

Huku kinyang’anyiro cha ubingwa wa ligi kuu ya premia nchini UIngereza ukielea ukingoni, ni maombi makubwa ya Arsenal kwamba West Ham itatenda haki kwa kuipiga Manchester City huku wao pia wakitazamia kuipiga Everton ili kutwaa ubingwa wa msimu huu.

Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta ametoa maoni yake akisema kwamba ni matumaini makubwa kwa kila mtu katika klabu hiyo kwamba Man City itateleza itakapomenyana na West Ham katika mechi ya kufunga msimu.

Arteta alisema kwamba si maajabu kwa West Ham kuipiga Man City, huku akimtegemea pakubwa David Moyes, ambaye alimleta Arteta kama mchezaji katika klabu ya Everton mwaka 2005, kumsaidia kunyanyua ubingwa kwa kuisimamisha City.

“Matumaini yapo. Haikufanyika [Spurs kushinda]. Sasa tunapaswa kufanya kazi yetu,” Mikel Arteta aliambia ripoti Ijumaa.

"Everton wako katika wakati mzuri sana, tunapaswa kuthibitisha tena kwamba tunaweza kuwa bora zaidi kuliko mpinzani na kisha kutamani bora, kwa West Ham kuwa na mchezo mzuri, kutusaidia na kutimiza ndoto zetu."

Kumbuka kuwa Arsenal vs Everton, na Man City vs West Ham United michezo itaanza saa 4 asubuhi. Jumapili, Mei 19, wakati huo huo.

Wakati huo huo, ziara ya haraka katika kurasa mbalimbali za mitandao ya kijamii ya West Ham ziliona mashabiki wengi wa Arsenal wakiirai timu hiyo kufanya haki kwa kuipiga City.

Chapisho ambalo West Ham walilochapisha kwenye ukurasa wake wa Facebook wakiwaonyesha vijana wake wakiwa mazoezini limefurika maoni kutoka kwa mashabiki wa Arsenal.

 Wengine walilenga wachezaji fulani, huku wengine wakitoa ofa za 'kichaa' ili kuwahamasisha The Hammers kuifunga City.

Newton Prince Okumu alisema: "Nilianza kushabikia Westham kabla sijazaliwa, ninyi ni timu kubwa duniani yenye kikosi cha thamani, Antonio ni bora kuliko Halaand, Lucas Paqueta ni bora kuliko Debruyen, Bowen ni bora kuliko Barnardo silver na Foden, Fabianski kama si David Raya ungeshinda glovu ya dhahabu, weka bao safi Jumapili na tutakualika kusherehekea nasi katika uwanja wa Emirates, tunakupenda Westham.”

Constant Jonns alisema: "Hata hivyo ni kinyume chako lakini ninaamini unaweza kumuaga Moyes."

Nigatu NG alisema: "Do for Rice ni legend of Hammers."

Tafwisamate alisema: "Wamehama kutoka ukurasa wa Spurs hadi hapa.”