•Katika pambano la fainali lilipigwa Wembley, magoli mawili ya ManUnited yalifungwa na Alejandro Garnacho na Kobbie Mainoo
Manchester United imetwaa ubingwa wa Kombe la FA kwa ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya mahasimu wao Manchester City likiwa ni taji lao la 13 mshindano hayo, taji moja pungufu ya Arsenal.
Katika pambano la fainali lilipigwa kwenye dimba la Wembley, magoli mawili ya Manchester United yamefungwa na Alejandro Garnacho na Kobbie Mainoo, huku kukiwa na goli pekee la Manchester City lililofungwa na Jeremy Doku.
Si tu kombe la FA ambalo Manchester United wamenyakua kwa ushindi huu, pia watacheza mashindano ya Ligi ya Uropa msimu ujao.
Kocha wa Man United, Erik ten Hag amelazimika kujibu maswali mengi na hakika amesikia mengi kuhusu mustakabali wake wikendi hii kwani bado hakuna uhakika iwapo atakuwepo msimu ujao hususan kutokana na kumaliza nafasi ya nane katika Ligi Kuu ya England.