logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Chelsea yamteua Enzo Maresca kama kocha mkuu

Enzo Maresca ameteuliwa kama kocha mkuu wa Chelsea kwa mkataba wa miaka mitano.

image
na Radio Jambo

Habari28 May 2024 - 13:00

Muhtasari


• Maresca amesaini mkataba wa miaka mitano na uwezekano wa kuzidisha hadi sita,hii ikionyesha  maono ya muda mrefu ya klabu.

• Meneja wa zamani wa Leicester City,Maresca alichaguliwa juu ya Thomas Frank, Kieran McKenna, na Robert De Cerbi ambao walikuwa pia kwenye hatua ya kuchaguliwa.

Chelsea wamekubali kumteua meneja wa Leicester City Enzo Maresca kama meneja wao mpya  kwa mkataba wa miaka mitano.

Muitaliano huyo anakuwa meneja wa nne wa kudumu wa enzi za Todd Boehly na Behdad Eghbali tangu klabu hiyo kuchukuliwa mwaka 2022. Wafuasi walisalia kwa mshtuko baada ya uongozi wa The Blues kuamua kuachana na Mauricio Pochettino mwishoni mwa msimu wa 2023/24, kufuatia kuimarika kwa fomu Stamford Bridge.

Hata hivyo, Pochettino aliondoka katika klabu hiyo kwa makubaliano baada ya kumalizika kwa msimu huu.Eghbali na wakurugenzi wa michezo Laurence Stewart na Paul Winstanley walianza mchakato kamili wa kumteua mrithi wake. Maresca, Thomas Frank, Kieran McKenna na Roberto De Zerbi wote walikuwa kwenye kinyang'anyiro hicho.

Kulingana na ripoti ya Fabrizio Romano,Maresca ametia saini mkataba wa miaka mitano na klabu hiyo huku kukiwa na chaguo la kuzidisha  hadi sita ambalo linaweza kumfanya asalie hadi Juni 2030.Hii inaonyesha mawazo ya muda mrefu ya The Blues na uteuzi huo.

Kocha huyo wa zamani wa Leicester City anaingia kazini baada ya kuiongoza Leicester kutwaa ubingwa na kupandishwa daraja la kwanza la Uingereza.

Kutashuhudiwa ubabe kuona jinsi msaidizi huyo wa zamani wa Manchester City anavyofanya kazi kama kocha mkuu katika Ligi ya Primia kwa mara ya kwanza. Matarajio moja ya kufurahisha ya kuzingatia ni kwamba amefanya kazi na Cole Palmer hapo awali, na kwa hivyo anaweza kufaa kupata bora kutoka kwa nyota huyo  wa "The Blues"

Ikumbukwe pia Arteta alitokea kama msaidizi wa Guardiola,na amekisuka kikosi cha Arsenal kwa ustadi mkubwa.Je,Maresca ataweka matumaini ya Chelsea kurejea kwenye ligi ya mabingwa kama hapo awali?


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved