Mikel Arteta ashinda tuzo ya Kocha Bora EPL 2023/24

Kocha wa Arsenal,Mikel Arteta ameshinda tuzo ya kocha bora wa ligi kuu ya Uingereza 2023/24 kwenye tuzo za Globe Soccer Awards zilizofanyika usiku wa Jumanne 28,Mei 2024.

Muhtasari

•Mikel Arteta alikabidhiwa tuzo ya kocha bora wa ligi kuu ya Uingereza 2023/24 na kiungo wa zamani wa Arsenal,Cesc Fabregas.

•Washindi wengine katika tuzo hizo walikuwa Kylian Mbappe, ambaye alikabidhiwa kama  mchezaji bora wa wanaume, Xabi Alonso-Kocha Bora, na Harry Kane aliyeshinda kama mfungaji bora

Mikel Arteta. Picha:Twitter
Mikel Arteta. Picha:Twitter

Meneja wa Arsenal Mikel Arteta alishinda tuzo ya Kocha Bora wa ligi kuu ya Uingereza kwenye tuzo za Globe Soccer Jumanne, akiwaambia watazamaji timu yake inaamini inaweza kushinda mataji.

Tuzo za Globe Soccer  zilifanyika Jumanne Mei 28,2024 na mkufunzi wa Arsenal Mikel Arteta alihudhuria akitarajia kushinda tuzo ya kocha bora wa ligi kuu ya 2023/24. Ingawa washindi wa ligi Manchester City walishinda tuzo ya klabu bora ya wanaume,Arteta alipokea tuzo ya kocha bora wa ligi kuu baada ya kura ya mashabiki.

Arteta alipokea tuzo hiyo kutoka kwa kiungo wa zamani wa Arsenal Cesc Fabregas, kabla ya kutoa hotuba kwa waliohudhuria.

"Tunataka kushinda," Arteta alisema kuhusu timu yake ya Arsenal "Hiyo ndiyo tunayotaka.Tuna timu iliyojaa ari na njaa ya kushinda mataji, tunaamini tunaweza kufanya hivyo... Kwa hivyo tutaifanyia kazi kweli."

The Gunners waliburuza mkia nyuma ya Manchester City, wakimaliza nafasi ya pili kwenye ligi kwa misimu miwili iliyopita. Walakini, chini ya uongozi wa Arteta, Arsenal imepata mafanikio makubwa, huku timu ikifurahia moja ya kampeni zao bora zaidi za ligi kuu msimu wa 2023/24. Wakijikusanyia pointi 89, Arsenal walipungukiwa tu na rekodi yao ya pointi walizoweka wakati wa msimu maarufu wa Invincibles wa 2003/04.

Zaidi ya hayo, walipata rekodi ya ushindi 28 kati ya mechi 38 na kufunga mabao 91 huku wakiendeleza rekodi ya kutoshindwa dhidi ya timu za ‘Big Six’. Arsenal inajiandaa kwa dirisha dogo la usajili la majira ya kiangazi huku wakipania kuimarisha kikosi chao katika kutafuta taji lao la kwanza la ligi tangu 2004.

Wakati huo huo, kupata ahadi ya muda mrefu ya Arteta kwa klabu ni kipaumbele, na mkataba wa Mhispania huyo unakamilika mnamo 2025. Washindi wengine katika tuzo hizo walikuwa Kylian Mbappe, ambaye alikabidhiwa kama  mchezaji bora wa wanaume, Xabi Alonso aliyetajwa kuwa Kocha Bora, na Harry Kane aliyeshinda kama mfungaji bora.