Mbappe atemwa nje kwenye kikosi cha muda kilichotajwa na Thiery Henry

Thiery Henry amemweka nje Kylian Mbappe baada ya kukitaja kikosi cha muda kitakachoshiriki mashindano ya michezo ya Olimpiki mwaka huu kule Paris .

Muhtasari
  • Kylian Mbappe ametemwa nje kwenye kikosi cha muda kilichotajwa na Thiery Henry kwenye mashindano ya michezo ya Olimpiki mwaka huu.
  • Sheria za mashindano hayo zinasema kwamba kila timu lazima iwe na wachezaji waliozaliwa mnamo au baada ya Januari 1, 2001
  •  Hata hivyo, wachezaji watatu waliozaliwa kabla ya tarehe hiyo wanaweza pia kujumuishwa.
Kylian Mbappe
Image: Hisani

Kylian Mbappé hajatajwa katika kikosi cha awali cha kocha mkuu wa Ufaransa Thierry Henry cha wachezaji 25 kwa ajili ya michezo ya Olimpiki jijini Paris msimu huu.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, ambaye anatarajiwa sana kujiunga na Real Madrid baada ya kumalizika kwa mkataba wake huko Paris Saint-Germain, alisema Machi 22 kwamba ana matumaini ya kushiriki katika michezo hiyo.

Henry alipendekeza katika mkutano na wanahabari Jumatatu kwamba Mbappé alikuwa hajaruhusiwa kucheza Olimpiki ya nyumbani kwake na klabu yake.

"Real Madrid walikuwa wawazi sana kuhusu Olimpiki," Henry alisema.

Henry aliweza kuwajumuisha wachezaji wawili wa Crystal Palace Michael Olise na Jean-Philippe Mateta katika orodha yake ya wachezaji, huku Mathys Tel wa Bayern Munich na kiungo wa kati wa PSG mwenye umri wa miaka 18 Warren Zaïre-Emery pia wakitajwa kwenye kikosi. Khéphren Thuram,kaka wa mshambuliaji wa Inter Milan Marcus Thuram, pia atashiriki.

Sheria za mashindano zinasema kwamba kila timu lazima iwe na wachezaji waliozaliwa mnamo au baada ya Januari 1, 2001 (wenye umri wa miaka 23 ) Hata hivyo, wachezaji watatu waliozaliwa kabla ya tarehe hiyo wanaweza pia kujumuishwa.

Kikosi cha muda cha Ufaransa cha wachezaji 25 kwa michezo ya Olimpiki:

Makipa: Lucas Chevalier, Obed Nkambadio, Guillaume Restes, Robin Risser

Mabeki: Bafodé Diakité, Maxime Estève, Bradley Locko, Castello Lukeba, Kiliann Sildillia, Adrien Truffert, Leny Yoro

Viungo wa kati: Maghnes Akliouche, Joris Chotard, Desiré Doué, Manu Koné, Enzo Millot, Khéphren Thuram, Lesley Ugochukwu, Warren Zaïre-Emery

Washambuliaji: Bradley Barcola, Arnaud Kalimuendo, Alexandre Lacazette, Jean-Philippe Mateta, Michael Olise, Mathys Tel