logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Chelsea yaweka wazi msimamo wa Romelu Lukaku

Chelsea yatangaza kumuachilia Lukaku huku ikikataa ofa zote za mkopo kwa mbelgiji huyo.

image
na Davis Ojiambo

Michezo06 June 2024 - 12:19

Muhtasari


  • •Romelu Lukaku anatazamiwa kuondoka Chelsea huku timu hio ikikataa ofa zote za mkopo  kutoka kwa vilabu vingine.
  • •Lukaku alisajiliwa kutoka Intermilan mwaka wa 2021 baada ya ubora wake ila mambo hayakuwa sawa ugani stamford bridge.

Chelsea itakataa ofa zote za mkopo kwa Romelu Lukaku kwa kuwa wanataka kumtoa kabisa msimu huu wa joto.

Mbelgiji huyo alirejea Stamford Bridge baada ya muda wake wa mkopo kule Roma kukamilika. Huu ukiwa ni msimu wake wa pili mfululizo mbali na 'The Blues' kuwa na mwaka mmoja ndani ya Inter Milan kabla ya hapo.

Chelsea ililipa £97.5M ambayo ilikuwa rekodi ya klabu ili kumnasa Lukaku mwaka 2021 lakini alishindwa kufikia matarajio na akaruhusiwa kuondoka baada ya miezi 12 pekee.Kwa sasa klabu hio kutoka magharibi mwa London wanataka kumwondolea mshahara wake wa pauni 325,000 kwa wiki kutoka kwenye vitabu vyao.Hii ikiwa na maana kuwa watakubali karibu pauni milioni 37,kutoka kwa klabu yoyote,kulingana na ripoti ya  BBC.

Baadhi ya vilabu kama vile AC Milan na Napoli wameonyesha ari ya kumsajili raia huyo wa Ubelgiji  lakini hawana uwezo wa kifedha na hawawezi kufikia bei inayotakiwa.Mshambulizi huyo amefanya kazi na  Antonio Conte ambaye ameteuliwa kama kocha mkuu wa Napoli.Wawili hao walishinda taji la Serie A kule Intermilan.

Aidha,Napoli walipendekezwa kuweka mkataba wa kubadilishana mshambuliaji Victor Osimhen, lakini Chelsea hawana nia ya kumsajili ,ambaye thamani yake ni zaidi ya £100m.

Kocha mwingine wa zamani wa Lukaku, Jose Mourinho, amesema hana nia ya kumleta fowadi huyo kwenye klabu yake mpya. Mourinho hivi majuzi aliteuliwa kuwa kocha wa Fenerbahce na amesisitiza kuwa hataleta mchezaji wake yeyote wa zamani nchini Uturuki.Mourinho amefanya kazi na Lukaku wakiwa Roma.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 alizifumania nyavu kwa ustadi mkubwa wakati alipokuwa Everton, Manchester United na Inter. Kule  San Siro alifunga  mabao 30  kwa  msimu, lakini katika kampeni yake pekee akiwa Chelsea alifunga mabao manane pekee ya ligi.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved