James Maddison aachwa nje kwenye kikosi cha wachezaji 26 cha England

Gareth SouthGate anatarajiwa kuwaondoa wachezaji wengine sita ili kufikia idadi ya wachezaji 26 kabla ya mashindano ya Euro 2024.

Muhtasari

•James Maddison ni mchezaji wa kwanza kati ya saba ambao wanatarajiwa kuondolewa kwenye kikosi cha Uingereza kabla ya mashindano ya Euro 2024.

•Kikosi cha wachezaji 26 ndicho kinachotarajiwa kutua nchini Ujerumani kwenye mahindano hayo ya msisimuko.

James Maddison
Image: X

James Maddison ameachwa nje ya kikosi cha wachezaji 26 cha England kwa ajili ya Euro 2024 na ameondoka kwenye kambi.

Kiungo huyo wa kati wa Tottenham aliitwa na kocha mkuu wa Uingereza, Gareth Southgate kwenye uteuzi wa muda wa wachezaji 33.Maddison alishiriki mechi ya  kirafiki ya England dhidi ya Bosnia-Herzegovina siku ya Jumatatu, akitokea benchi katika ushindi wa 3-0 kwenye Uwanja wa St James' Park.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 amechezea Uingereza mechi saba  na alikuwa sehemu ya kikosi cha Southgate kwa Kombe la Dunia la 2022, ingawa hakupewa muda wa kucheza kule Qatar.

Huenda mchezo wa Eberechi Eze na Cole Palmer dhidi ya Bosnia uliyumbisha fikra za Southgate.Wawili hao walionyesha mchezo wa wakuvutia kwenye mechi ya kirafiki na wanaweza kuwa juu ya Madisson kulingana na  Southgate kutokana na kupanga mpira kwenye safu ya kati.

Maddison alijiunga na Tottenham kwa uhamisho wa pauni milioni 40 kutoka Leicester msimu uliopita.Kiungo huyo alikuwa na mwanzo mzuri  ugani Tottenham Hotspurs hadi wakati   jeraha lilipomkumba hivyo viwango vyake vya mchezo kuburura kwa kiasi.

Kikosi cha mwisho cha England kwa ajili ya michuano hiyo kitatangazwa Jumamosi, baada ya mechi yao ya mwisho ya kirafiki ya kujiandaa  dhidi ya Iceland kwenye uwanja wa Wembley,huku Southgate akitarajiwa kuwaondoa wachezaji sita kwenye kikosi hicho ili kufikia 26.

Aidha Luke Shaw hajaondolewa kikosini licha ya kuwa na jeraha ambalo limemweka nje kwa msimu,kule Manchester United.