Kocha wa Harambee Stars Engin Firat, atumainia ushindi dhidi ya Burundi

Kenya itamenyana na Burundi Ijumaa kabla ya kumenyana na Ivory Coast Jumanne

Muhtasari

•"Sikati tamaa na wavulana pia hawakati tamaa. Lengo letu ni kwa wachezaji tulio nao hapa kujaribu tuwezavyo kupata pointi tatu,” aliongeza Firat.

• Mechi hiyo itafanyika Ijumaa alasiri huku Kenya ikicheza mechi zao za nyumbani ugenini Malawi kutokana na ukosefu wa uwanja ulioidhinishwa nchini Kenya.

Kocha wa Harambee Stars
Kocha wa Harambee Stars, Engin Firat Kocha wa Harambee Stars
Image: Facebook

Kocha wa Harambee Stars Engin Firat, ametoa ufahamu kuhusu anachotarajia kutoka kwa wapinzani wa Kenya, Burundi, wakati wa mchuano wa mechi ya Ijumaa ya kufuzu kwa Kombe la Dunia la mwaka 2026.

Firat, anatarajia Burundi kucheza mchezo wa mashambulizi wakati pande hizo mbili zitamenyana kwenye mechi yao ya kufuzu kwa Kombe la Dunia la 2026 mnamo Ijumaa.

Kenya itamenyana na Burundi katika mechi ya kwanza kati ya mbili ya kufuzu kwa Kombe la Dunia kwenye uwanja wa taifa wa Bingu Lilongwe, Malawi huku kila timu ikitarajia kushinda mechi hiyo.

Firat anapanga kutumia mtindo wa tahadhari dhidi ya Burundi kwa msisitizo wa kupata uwiano sawa kati ya ulinzi na mashambulizi ili wapinzani wao wasiwaadhibu.

"Tunakabiliwa na mpinzani ambaye ana mchezo mkali sana wa mpito, wanacheza kwa kasi sana kutoka kwa kina, wana wachezaji wengi wenye kasi."

"Kwa hivyo, ninahisi watatumia nafasi wanayoweza kupata ikiwa tutawakandamiza na kujaribu kupata mipira mirefu nyuma ya safu yetu ya ulinzi ila tumejiandaa vilivyo,” alisema Firat Alhamisi.

Mkufunzi huyo wa Uturuki, hata hivyo, ana uhakika wa kupata pointi nyingi zaidi kutokana na mechi hiyo ambayo itaimarisha sana matumaini ya timu yake ya kufuzu Kombe la Dunia kabla ya kuvaana na Ivory Coast siku ya Jumanne.

"Sikati tamaa na wavulana pia hawakati tamaa. Lengo letu ni kwa wachezaji tulio nao hapa kujaribu tuwezavyo kupata pointi tatu,” aliongeza Firat.

Firat afichua malengo makubwa ya Harambee Stars baada ya maandalizi yake kuimarika nchini Malawi. Mechi hiyo itafanyika Ijumaa alasiri huku Kenya ikicheza mechi zao za nyumbani ugenini kutokana na ukosefu wa uwanja ulioidhinishwa nchini Kenya.

Hata hivyo, kikosi kinajaa matumaini kabla ya mtihani mkubwa unaowasubiri.

Kenya, sawa na Burundi, wana pointi tatu katika mechi zao mbili za kwanza, kufuatia kipigo cha 5-0 kutoka kwa Ushelisheli, na kupoteza 2-1 nchini Gabon, huku wapinzani wao wakiicharaza Gambia na kushindwa na Gabon.