logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Euro 2024: Hali ya Mbappe sio nzuri huku Slovakia ikiishangaza Ubelgiji

Diallo aliwaambia waandishi wa habari mjini Duesseldorf kwamba Mbappe "hahitaji kufanyiwa upasuaji", kiwango cha jeraha lake bado hakijajulikana.

image
na SAMUEL MAINA

Michezo18 June 2024 - 04:22

Muhtasari


  • •Rais wa Shirikisho la Soka la Ufaransa, aliwaambia waandishi wa habari mjini Duesseldorf kwamba Mbappe "hahitaji kufanyiwa upasuaji", kiwango cha jeraha lake bado hakijajulikana.

Kocha wa Ufaransa Didier Deschamps amesema nahodha Kylian Mbappe "hayuko vizuri" baada ya kuoata jeraha baya la pua katika ushindi wao wa 1-0 dhidi ya Austria Jumatatu.

Wakati Philippe Diallo, rais wa Shirikisho la Soka la Ufaransa, aliwaambia waandishi wa habari mjini Duesseldorf kwamba Mbappe "hahitaji kufanyiwa upasuaji", kiwango cha jeraha lake bado hakijajulikana.

Mwishoni mwa mchezo wa ufunguzi wa Euro 2024 wa Ufaransa mjini Düsseldorf, Mbappe alipiga mpira kwa kichwa na uso wake ukagonga bega la Kevin Danso katika pasi ya kufuatisha.

Fowadi huyo mwenye umri wa miaka 25 alipokea matibabu uwanjani, akiwa na damu nyingi usoni, na kisha akatoka nje ya uwanja huku Ufaransa ikitaka kumtoa ili nafasi yake kuchukuliwa na Olivier Giroud.

Mchezo ulipoanza tena, Mbappe alienda uwanjani bila ruhusa na kuketi - hatua iliyomfanya kupewa kadi ya njano.

Nafasi yake ikachukuliwa na Giroud.

"Haendelei vizuri," bosi Didier Deschamps alisema katika mkutano wa waandishi wa habari baada ya mechi.

Kwingineko Slovakia ilizua taharuki katika mechi yao ya ufunguzi ya Euro 2024 ilipowashangaza Wabelgiji katika Kundi E kwa kuwashinda bao 1-0 katika mchuano mkali mjini Frankfurt.

Kulikuwa na hali mbaya katika dakika za mwisho ambapo Romelu Lukaku alidhani alisawazisha, lakini (VAR) ikakataa bao hilo na kusema mpira ulishikwa kwa mikono wakati wa maandalizi.

Lilikuwa ni bao la pili alilofunga ambalo lilikataliwa na VAR baada ya hapo awali kuunganisha kwa kichwa mpira wa kichwa kutoka kwa Amadou Onana.

Ivan Schranz aliiweka Slovakia mbele alipotumia vyema makosa ya Jeremy Doku wa Manchester City.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved