CR7 na Pepe waandikisha rekodi mpya kwenye mashindano ya Euro 2024 nchini Ujerumani

Akiwa kwa mara ya kwanza kwenye kikosi cha Ureno mwaka 2004, Ronaldo alicheza mechi yake ya kwanza ya Euro kwenye ardhi ya nyumbani, akifunga bao lake la kwanza kwenye michuano hiyo dhidi ya Czech.

Muhtasari

• Ronaldo, 39, tayari ana rekodi ya kucheza mechi nyingi za Euro (26), mabao (14) na mabao katika matoleo matano ya michuano hiyo.

• Pepe mzaliwa wa Brazil alikuwa na umri wa miaka 24 alipocheza mechi yake ya kwanza Ureno chini ya kocha Mbrazil Luiz Felipe Scolari mnamo Novemba 2007.

PEPE NA CR7
PEPE NA CR7

Cristiano Ronaldo amekuwa mchezaji wa kwanza wa wanaume kushiriki michuano sita ya Ulaya alipoiongoza timu yake kushinda 2-1 dhidi ya Jamhuri ya Czech katika michuano ya Euro 2024 ya Kundi F.

Wakati huo huo, mwenzake Pepe pia aliweka rekodi ya kuwa mchezaji mkongwe Zaidi kuwahi kushiriki mashindano ya Euro, akiwa na umri wa miaka 41 na siku 113.

Akiwa kwa mara ya kwanza kwenye kikosi cha Ureno mwaka 2004, Ronaldo alicheza mechi yake ya kwanza ya Euro kwenye ardhi ya nyumbani, akifunga bao lake la kwanza kwenye michuano hiyo dhidi ya Czech.

 Sasa, miaka 20 baadaye, Ureno ilikabiliana na timu hiyo tena katika mechi yao ya ufunguzi ya michuano ya sita ya Ronaldo.

"Leo inaanza sura nyingine katika historia yetu. Naikumbuka vyema siku yangu ya kwanza na timu ya taifa, safari iliyojaa changamoto na ushindi. Sasa, nina heshima ya kuwa pamoja na timu ya mabingwa, iliyojaa vipaji na dhamira," Ronaldo alichapisha kwenye mtandao wa kijamii wa X.

Ronaldo, 39, tayari ana rekodi ya kucheza mechi nyingi za Euro (26), mabao (14) na mabao katika matoleo matano ya michuano hiyo.

Pepe mzaliwa wa Brazil alikuwa na umri wa miaka 24 alipocheza mechi yake ya kwanza Ureno chini ya kocha Mbrazil Luiz Felipe Scolari mnamo Novemba 2007 alipokuwa bado mchezaji wa Real Madrid.

Ameichezea Ureno mechi 138, akifunga mabao nane, na kupata kadi 25 za njano.

Kadi yake moja nyekundu ilipatikana katika mchezo wa ufunguzi wa Ureno kwenye Kombe la Dunia 2014 dhidi ya Ujerumani.