Euro 2024:Mashabiki watatu wa Uingereza watiwa mbaroni

Mashabiki hao walikamatwa kabla ya mechi yao dhidi ya Denmark kwenye mashindano ya Euro.

Muhtasari

•Mashabiki watatu wa Uingereza walikamatwa baada ya shabiki mmoja kudhulumu polisi,mwingine kwa kuhusika na dawa za kulevya huku wa tatu kwa kurusha chupa.

•Aidha,polisi wa Ujerumani walisifia mashabiki wengi wa Uingereza kuwa na tabia nzuri japo tu watatu hao.

Mashabiki watatu wa Uingereza wamekamatwa na polisi wa Ujerumani kabla ya mechi ya Alhamisi  dhidi ya Denmark mjini Frankfurt.

Vijana wa Gareth Southgate wanakutana na Denmark katika mechi yao ya pili ya kundi C uwanjani Frankfurt Arena. Three Lions  wako katika nafasi nzuri kuelekea mchezo huo baada ya kuifunga Serbia Jumapili na ushindi mwingine unaweza kuwafanya wafuzu kwa hatua ya kumi na sita bora.

Wafuasi wengi wamekuwa na tabia nzuri, sasa imeibuka kuwa watatu walikamatwa usiku wa kuamkia kabla ya mechi hiyo. Polisi walithibitisha kuwa mtu mmoja alikamatwa kwa kumdhulumu afisa wa Uingereza na mwingine kwa kurusha kombora na kuwa na dawa za kulevya.

Mfuasi wa tatu alikamatwa kwa kurusha chupa. Kitengo cha polisi cha Kandanda cha Uingereza (UKFPU), ambao wako Ujerumani, wanakadiria kuwa karibu mashabiki 2000 wa Uingereza walikuwa nje katika uwanja kuu Jumatano usiku.

"Takriban mashabiki 2,000 wa Uingereza walikuwa katika uwanja mkuu wa jiji la Frankfurt jana usiku (Juni 19) na hakuna masuala makubwa yaliyoripotiwa," taarifa hiyo ilisoma.

"Hii ni dalili ya kile ambacho tumekiona kote Ujerumani hadi sasa, na idadi kubwa ya mashabiki wa England wana tabia nzuri sana. Mashabiki watatu wa Uingereza walikamatwa na polisi wa Ujerumani..."