Winga wa Bayern Munich Leroy Sane amekiri majuto yake makubwa tangu alipokuwa Manchester City baada ya kuweka tattoo kubwa kwa mgongo wake.
Winga huyo mwenye umri wa miaka 28 yuko pamoja na kikosi cha Ujerumani kujaribu kuwasaidia kutwaa ubingwa wa Euro 2024 kwenye uwanja wa nyumbani.
Mojawapo ya nyakati nzuri zaidi kwa Sane ni wakati alipofungia Manchester City katika ushindi wa 5-3 wa ligi ya mabingwa dhidi ya Monaco.
Nyota huyo wa zamani wa Schalke 04 alijichora tattoo kuadhimisha bao hilo, lakini sasa anatamani asingefanya hivyo.
Akizungumza na Der Spiegel, Sane alisema: “Kama nilivyosema, nilikuwa mdogo. Leo ningefanya uamuzi tofauti."
"Nilikuwa mtu ambaye alilazimika kukimbilia ukutani angalau mara moja, hata ikiwa iliumiza, ili kujifunza kutoka kwake, haswa katika umri mdogo." Sane aligonga vichwa vya habari alipofichua kazi hiyo ya sanaa mnamo 2017.
Jambo ambalo anakiri lilimshangaza. Alisema:
“Nilishangaa kuwa mada hii ilikuwa kubwa kwenye vyombo vya habari, nilikuwa bado kijana mdogo ...nchini Ujerumani kulikuwa na wachezaji muhimu zaidi kuliko mimi, na bado tattoo hii ilikuwa bado inajadiliwa. Marafiki wameniambia hivyo pia: 'Leroy, watu fulani husema kwamba unajiona kuwa mtu mwenye kiburi.' Naweza kuelewa hata kidogo. “Ninapokuwa hadharani, huwa najitenga. Sitaki kufichua mengi kunihusu. "Hiyo inaweza kutokea vibaya. Sio makusudi. Na mimi siko hivyo pia.”
Sane aliondoka Etihad mwaka 2020 na kurejea katika ligi ya nyumbani kwao kule Ujerumani. Tangu wakati huo ameshinda Bundesliga mara tatu pamoja na kombe la klabu bora duniani, 'Uefa Super Cup' na tatu za 'Super Cup' za Ujerumani.
Mchezaji huyo atakuwa anawinda kuongeza idadi ya mabao katika timu ya taifa ya Ujerumani katika mashindano ya Euro 2024 baada ya kufumania jumla ya mabao 13 wakati Ujerumani itamenyana na Denmark katika hatua ya 16 bora Juni 29.