Sajili mpya wa Chelsea Kiernan Dewsbury-Hall: Nafuata nyayo za Lampard na Kante

"lakini pia wachezaji kama Fabregas, Mata na hata Kante ambaye tulikuwa na yeye Leicester City " Dewsbury-Hall alisem.

Muhtasari

• "Ni dhahiri kwamba ninamjua kocha na jinsi anatutaka tucheze na pia kukosi hiki kimejaa talanta tupu."

 

Kiernan Dewsbury-Hall
Kiernan Dewsbury-Hall
Image: Chelsea

Mchezaji sajili mpya wa miamba wa London, Chelsea, Kiernan Dewsbury-Hall amefunguka kuhusu ndoto yake ya utotoni na jinsi baadhi ya wachezaji wa awali wa Chelsea walivyomvutia kwenye soka. 

Akizungumza na waandishi wa habari wa Chelsea siku moja baada ya utambulisho klabuni humo, Dewsbury-Hall alisema kwamba tangu utotoni, amekua akifuatilia uchezaji wa viungo wa kati wa Chelsea waliofana enzi zao.

Pia alisema kulichomvutia kuikataa Brighton na kuichagua Chelsea ni ukaribu wake ba kocha mpya wa Chelsea, Enzo Maresca.

"Ni dhahiri kwamba ninamjua kocha na jinsi anatutaka tucheze na pia kukosi hiki kimejaa talanta tupu."

"Kuna wachezaji wengi wazuri ambao nimekuwa nikiwatazama tangu utotoni. Wa kwanza kabisa ni Frank Lampard, kiungo wa kati aliyezoea kufunga mabao; kitu ambacho ningependa kujaribu na kuifanya kuwa moja ya uchezaji wangu..."

"...lakini pia wachezaji kama Fabregas, Mata na hata Kante ambaye tulikuwa na yeye Leicester City " Dewsbury-Hall alisem.

Chelsea walimsajili Dewsbury-Hall kutoka Leicester kwa kitita cha pauni milioni 30 na kutia saini mkataba wa miaka 5 na Chaguo la mwaka mmoja zaidi.