Enzo Fernandez aongoza orodha ya jezi za Chelsea zilizonunuliwa zaidi msimu uliopita

Nafasi ya pili ilishikiliwa na nahodha Reece James ambaye jezi yake ya nambari 24 mgongoni iliwavutia wengi licha ya kutumikia karibia msimu wote akiwa nje kutokana na jeraha.

Muhtasari

• Winga wa Ukraine Mykhailo Mudyryk alishika nafasi ya 5 katika mauzo ya jezi yake yenye nambari 10 mgongoni.

• Sajili mpya ambaye pia alikuwa mfungaji bora kwa klabu hiyo, Cole Palmer akishika nafasi ya nne kwa mauzo ya jezi yake ya nambari 20 mgongoni.

Wachezaji wa Chelsea waliouza jezi nyingi
Wachezaji wa Chelsea waliouza jezi nyingi
Image: CHELSEA TV

 Miamba wa soka kutoka London nchini Ungereza, Chelsea maarufu kama The Blues wametoa takwimu za jinsi jezi za wachezaji wao mbalimbali zilivyonunuliwa sokoni na mashabiki na wapenzi wa Chelsea.

Katika takwimu hiyo, Chelsea walitoa orodha ya wachezaji 5 wa kwanza ambao jezi zao zilikuwa zinanunuliwa sokoni bila kukawia.

Winga wa Ukraine Mykhailo Mudyryk alishika nafasi ya 5 katika mauzo ya jezi yake yenye nambari 10 mgongoni huku sajili mpya ambaye pia alikuwa mfungaji bora kwa klabu hiyo, Cole Palmer akishika nafasi ya nne kwa mauzo ya jezi yake ya nambari 20 mgongoni.

MYKHAILO MUDRYK
MYKHAILO MUDRYK
COLE PALMER
COLE PALMER

Nambari ya tatu ilishikiliwa na mkongwe Thiago Silva na jezi yake nambari 6 mgongoni, ambaye alifanya kazi kubwa kuhimiza klabu hiyo kumaliza katika nafasi ya 6 kwenye msimamo wa jedwali.

Silva, 39, ambaye aliondoka kishujaa mwishoni mwa msimu alimiminiwa sifa kwa kuonyesha uongozi na uzoefu wake kwa timu hiyo ambayo ilikuwa na asilimia kubwa ya wachezaji wachanga chini ya umri wa miaka 25.

THIAGO SILVA
THIAGO SILVA

Nafasi ya pili ilishikiliwa na nahodha Reece James ambaye jezi yake ya nambari 24 mgongoni iliwavutia wengi licha ya kutumikia karibia msimu wote akiwa nje kutokana na jeraha.

James alirejea mwishoni mwa msimu na kushiriki mechi mbili kabla ya kuonyeshwa kadi nyekundu ambayo itamfungia mechi 4 za ufunguzi wa msimu ujao wa mwaka 2024/25.

REECE JAMES
REECE JAMES

Katika nafasi ya kwanza, kiungo wa kati Muargentina Enzo Fernandez aliongoza kwa mauzo mengi ya jezi yake nambari 8 mgongoni.

Licha ya kusuasua kwa baadhi ya mechi, Enzo Fernandez bado anachukuliwa kama moja ya hazina kuu na yenye thamani kwa klabu ya Chelsea na anatarajiwa kuipata fomu yake nzuri chini ya kocha mpya Enzo Maresca msimu huu.

ENZO FERNANDEZ
ENZO FERNANDEZ

Chelsea walifaulu katika kumshawishi Enzo Fernandez kutoshiriki mechi za Oimpiki na timu ya taifa la Argentina ambazo zitang’oa nanga mwezi kesho nchini Ufaransa.

Lengo lao lilikuwa kwamba Fernandez awe mmoja wa wachezaji ambao wataanza mazoezi na mechi za kujifua kuelekea msimu mpya.