logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Foden ametaka wachezaji kulaumiwa na wala si kocha Southgate

Phil Foden amewataka wachezaji wa Uingereza kubeba lawama na wala si Southgate kulaumiwa.

image
na Davis Ojiambo

Michezo04 July 2024 - 06:41

Muhtasari


  • •Phil Foden ametaka wachezaji wenzake kuonyesha uongozi bora kwenye mechi dhidi ya Uswizi ili kuondoa shinikizo kwa kocha mkuu Gareth Southgate.
  • •Foden amecheza jumla ya dakika 337 bila bao wala 'assist'  kwenye michuano ya Euro 2024 huku akianza kila mechi.
PHIL FODEN

Nyota wa timu ya Uingereza,Phil Foden amesema kuwa wachezaji wa Uingereza wanahitaji kubeba lawama kwa uchezaji wao wa kukatisha tamaa hadi sasa kwenye michuano ya Euro 2024 na kwamba "anamuhurumia" Gareth Southgate.

Katika mahojiano ya wazi, Foden alikiri kuwa "amechanganyikiwa" na jinsi yeye na Uingereza walivyocheza - "baadhi ya michezo haikuwa sisi" - na kuwataka wachezaji wenyewe kuonyesha uongozi bora kabla ya Jumamosi ya robo fainali dhidi ya Uswizi.

"Ninahisi kama wachezaji wanapaswa kuchukua lawama ..Lazima kuwe na baadhi ya viongozi ili kujumuika pamoja na kutafuta suluhu kwa nini haifanyiki kazi. Kuna mengi tu ambayo meneja anaweza kufanya." Foden alisema.

Kulingana na sports telegraph;Southgate amekosolewa vikali, kwa shutuma kwamba alitumia mbinu za kihafidhina na hapati matokeo bora kutoka kwa chaguzi za kusisimua za England, lakini Foden alisisitiza kuwa haikuwa kosa lake.

Foden mwenye umri wa miaka 24 alidai kuwa anamuonea huruma kocha mkuu Gareth Southgate;

“Namuonea huruma Gareth. Hajapanga kufanya hivyo,” Foden alisema.

"Katika mazoezi amekuwa akituambia tuimarike tukiwa  uwanjani na ninahisi kama wakati mwingine lazima itoke kwa wachezaji. Lazima tuwe viongozi na ninahisi kama katika michezo hiyo tungeweza kukusanyika zaidi kidogo na kupata suluhisho."

Aliongeza; "Sisi [wachezaji] tumezungumza zaidi juu yake na ikiwa itatokea tena kwenye mchezo, tunaweza kukusanyika na kutafuta suluhisho na kuona ni wapi inaenda vibaya na kurekebisha."

Foden alitolewa katika dakika ya 94 ya hatua ya 16 bora kwenye mechi kati England dhidi ya Slovakia,huku akiwa amecheza jumla ya dakika 337 bila bao wala 'assist'.

England ipo matayarishoni kumenyana na Uswizi kwenye hatua ya robo fainali katika michuano ya Euro 2024  Julai 6 2024.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved